Thursday, August 10, 2017

VIPINDI VYA KILIMO KATIKA VYOMBO VYA HABARI VITASAIDIA KUINUA KILIMO NCHINI

 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo mjini hapa leo. Mafunzo hayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB). Kutoka kushoto ni Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa Wilaya ya Mtwara, Joseph Tesha, Kaimu Katibu Tawala, Francis Mkuti na Mshauri wa Kilimo Mkoa wa Mtwara, Ally Linjenje.

 Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mtwara, George Mrisho, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
 Maofisa Ugani wakijitambulisha kwa mkuu wa wilaya hiyo ambaye alikuwa mgeni rasmi.
 Mkutano na maofisa ugani ukiendelea.
 Mafunzo yakitolewa.
 Mwezeshaji kutoka OFAB, Dk. Emmarold Mneney, akitoa mada kuhusu matumizi ya bioteknolojia na sayansi katika kilimo.
 Ofisa Kilimo Mohamed Kaid kutoka wilaya hiyo, akichangia jambo.
 Ofisa Kilimo kutoka Kata ya Msanga Mkuu, Maonyesho Bakari Said, akichangia katika mafunzo hayo.
 Ofisa Kilimo Hamidu Ndago kutoka wilaya hiyo, akichangia jambo.
 Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa Wilaya ya Mtwara, Joseph Tesha, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
 Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, Naliendele Mtwara, Benadetha Kimata, akitoa mada kuhusu kilimo bora  cha mhogo. 
Wawezeshaji wa mafunzo ya kutumia teknolojia katika kilimo kutoka COSTECH wakiwa kikazi zaidi katika mafunzo hayo. Kutoka kulia ni Mtafiti, Dk.Nicholaus Nyange, Rose Soloka na Bestina Daniel.

Na Dotto Mwaibale, Mtwara

MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda amesema vipindi vya kilimo katika vyombo vya habari vitasaidia kuinua sekta ya kilimo nchini.

Mmanda ameyasema hayo mjini hapa leo wakati akifungua mafunzo ya namna ya kutumia sayansi na teknolojia katika kuboresha kilimo kwa maofisa ugani kutoka  Halmashauri ya wilaya ya Mtwara na Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara ambayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB).

" Nitoe mwito kwa wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na Costech kuandaa vipindi kwa njia ya radio na televisheni na machapisho mbalimbali kama magazeti ili kuhamasisha kilimo bora jambo litakalosaidia kuinua sekta ya kilimo hapa nchini na vijana wataweza kujifunza kuhusu kilimo badala ya kuangalia vipindi vya visivyo na tija hasa katika wakati huu wa nchi yetu kuelekea katika uchumi wa viwanda" alisema Mmanda. 

Katika hatua nyingine Mmanda amewataka maofisa ugani katika wilayani wajenge mazoea ya kwenda kushinda na wakulima mashambani ili waweze kutoa utaalamu ambao utawezesha kupatikana kwa mazao mengi na bora.

Alisema haiwezekani mkulima kupata mazao bora bila kupatiwa ushauri na ofisa ugani na hivyo akasisitiza kuwa watalamu hao waache tabia ya kukaa maofisini, badala yake wakafanye kazi waliyoajiriwa ambayo ni kutoa ushauri kwa wakulima. 


Mmanda alisema  kilimo ni sayansi, hivyo kuna haja ya wagavi kupatiwa mafuzo ya mara kwa mara kutoka kwa watafiti ambao wamekuwa wanafanya tafiti mbalimbali za namna ya kuboresha kilimo huku akisisitiza ushirikiano kati ya mkulima, ofisa ugani na mtafiti kuwa ni muhimu. 


Mwezeshaji kutoka OFAB, Dk. Emmarold Mneney aliwaambia maofisa ugani hao kuwa wameamua kutoa mafuzo hayo kwa kuwa wanaamini kwamba changamoto zinazokabili kilimo ni nyingi hasa magonjwa ya mazao, wadudu waharibifu pamoja na kukosekana kwa mvua za kutosha.

Alisisitiza kuwa mkulima ili aweze kuwa na kilimo chenye tija, lazima uongezee udongo wako lishe, utibie mimea yako kama wewe unavyotibiwa na dawa ili yapone na yatoe mazao mengi. Alisema sayansi ipo kwa ajili ya kumfanya mkulima apate mazao mengine  na sio kuendelea kuwa maskini kama ilivyo sasa.

“Tuko hapa kuelezea namna teknolojia hizi ambazo zinasaidia kukabiliana na changamoto hizo, lengo ni kutaka wakulima wetu wazalishe kwa tija nchi ijitosheleze kwa chakula lakini pia mkulima auze mazao yake na kupata faida,” alisema Dk. Mneney.



No comments: