Naibu Waziri wa mambo ya ndani Mh. Hamad masauni amesifu jitihada zinazofanywa na safu ya Uingozi wa Chuo cha Taifa cha usafirishaji (N.I.T) chini ya Profesa Zacharia Mabubu Mganilwa, za kufua wataalamu wa nyanja mbalimbali katika sekta ya usafirishaji ikiwamo usafiri wa anga.
Masauni ameyasema hayo wakati alipotembelea chuo cha
taifa cha usafirishaji(NIT) na kujionea vitu mbalimbali ikiwepo kifaa
kinachotumika kuongoza ndege (flight simulator) pamoja na kituo kinachotumika kufanya ukaguzi wa magari (vehicle
inspection) ambacho tayari kimeanza kufanya kazi kikishirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Aidha kwa upande Mkuu wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Prof. Zacharia Mganilwa akielezea ufanisi wa kituo cha ukaguzi wa magari (vehicle inspection) amesema kituo hicho kinauwezo mkubwa wa kukagua magari.
"Tunashirikiana na wenzetu TBS katika kazi hii ya ukaguzi wa magari, wenzetu wanayaelekeza magari yote yanayonunuliwa kuja hapa kukaguliwa kabla hayajaanza kutumika katika barabara zetu...na kwa siku kituo chetu kina uwezo wa kukagua magali zaidi ya 600...lakini si hivyo tu pia vijana wengi wamepata ajira hususani wahandisi wa magari" . Alisema Prof Mganilwa
Naibu Waziri Masauni alikuwa katika ziara yake ya kawaida jana ambako aliweza kujionea maendeleo ya chuo cha taifa cha usafirishaji.
No comments:
Post a Comment