Monday, September 11, 2017

BILL NAS AFUNGUKA KUHUSU WATU WASIOJULIKANA

MKALI wa wimbo wa Sina Jambo, anayefahamika zaidi kwa jila la Bill Nas amefunguka kuwa hakuna kitu ambacho kinampagawisha kwa sasa kichwani kwake, kama matukio yanayofanywa na watu wasiojulikana.
Image result for invisible man
Akichonga na Showbiz, Bill Nas ambaye video ya wimbo wake huo mpya imetengenezewa Sauz na prodyuza Msafi ri alisema, mbali na kumpa pole Mwanasheria na Mbunge Tundu     Lissu wa tukio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana anatoa rai kwa jeshi la polisi ambao wanadhamana ya kusimamia usalama wa raia kuhakikisha wanakomesha matukio yanayofanywa na watu wasiojulikana.

“Kiukweli ukiwafi kiria watu wasiojulikana ni lazima upagawe.
Kwa sababu leo watu hao wamemfanyia unyama wa kutisha Lissu, ujui kesho uenda wakanifanyia mimi na wasichukuliwe hatua kwa sababu hawajulikani, kwa hiyo ifi ke hatua polisi wawafahamu hawa watu wasiojulikana!” Alisema Bill Nas.
     

No comments: