Shirika lenye
kutekeleza program na mipango mbalimbali yenye kukuza, kutetea na kuboresha
haki na ustawi wa mtoto wa Tanzania(CDF) Leo tarehe 26 mwezi septemba limefanya
mkutano wa mrejesho wa mradi wa kuhamasisha jamii kutokomeza ndoa za utotoni,
ukeketaji na mimba za utotoni katika kata ya kitunda manispaa ya Ilala.
Mradi huo
uliyofadhiliwa na ubalozi wa Uhoanzi ulianza kitunda kwani kata hiyo ilionekana
kuwa na kiwango kikubwa cha ukeketaji hali iliyofanya kuwepo kwa ndoa nyingi za
utotoni hivyo kitunda kuwa ya kwanza katika wilaya ya ilala hata kimkoa pia.
Mradi huo
ulitekelezwa kwa kuanzisha vilabu mashuleni, kwa kuanzisha midahalo kwa watoto,
vijana wakike na wakiume ambao ni wakazi wa kata ya kitunda ili kuwajengea uwezo wakazi
hao ili kufahamu madhara ya ukeketaji ili waweze kuwa mabarozi wazuri wa kulinda
na kutetea haki na ustawi wa mtoto wakike.
Njia nyingine
ilikuwa ni kupitia michezo imekuwa ni sehemu nzuri ya kuwavuta watu wengi na
hapo hapo walipata elimu hii haswa wanaume ambao ni watekelezaji wa kubwa wa
mimba za utotoni na kukiri kuacha tabia hiyo na kuahidi kuwa mabalozi wazuri
kwa wenzao ili kukomesha vitendo hivi vya ukeketaji, mimba pamoja na ndoa za
utotoni.
Lakini pia
njia nyingine ilikuwa ni kutumia vyombo vya habari kwa kufanya mikutano na
waandishi wa habari, kwenda katika mahojiano ya vipindi vya radio na
televisheni pamoja na magazeti na blogs mbalimbali.
Mgeni rasmi kitika
mkutano huo alikuwa ni Naibu Balozi wa Uholanzi Ms. Lianne Houben ambaye pia
alizindua tovuti ya rasmi ya CDF ambayo itakuwa ikiweka taarifa zote za miradi
inayoendeshwa na shirika hilo, lengo likiwa ni wananchi kutambua shughuli
zinazofanywa na shirika hilo na kupata elimu kuhusu ndoa za utotoni, mimba za
utotoni na ukeketaji wa wasichana na wanawake.
Miongoni mwa
faida za mradi huo ni wanafunzi kupenda sana vilabu hivyo na kujitokeza kwa
wingi katika ushiriki hivyo kupata elimu iliyokusudiwa na tangu kuanza kwa
mradi huo kumewajengea uwezo mzuri wanafunzi hao na kujilinda dhidi mambo
yasiyowafaa kwa umri wao ikiwa ni kupinga ukeketaji na ndoa na mimba za
utotoni.
Wanafunzi kuwa
tayari kutoka nje ya shule zao na kuipeleka elimu hiyo maeneo mengine ikiwemo
shule nyingine hata katika jamii inayowazunguka wakiwemo wazazi pamoja na
walezi ili wajue madhara ya ukeketaji na vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia.
Na faida
nyingine ni kubadilishana uzoefu kati ya waelimishaji pamoja na watoto hivyo
kuweza kugundua mambo mengi yanayowakabiri watoto ambayo ushindwa kuyaongea kwa
wazazi au jamii, kwa kushirikiana na walimu wao wamepata kujua mambo mengi
zaidi.
Naibu balozi wa Uholanzi Nchini Bi. Lianne Houben akibonyeza kitufe kuzindua wa Tovuti ya shirika la jukwaa la utu wa mtoto (CDF) pembeni yake ni Mkurugenzi mtendaji wa shirika la jukwaa la utu wa watoto (CDF), Bw.Koshuma Mtengeti jijini Dar es salaam. |
Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Kitunda Gladness Vitus kutoka CDF klabu akielezea namna ambavyo mradi huo una wanufaisha wanafunzi wa shule yao. |
Wanafunzi kutoa shule mbalimbali za kata ya kitunda wakifatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo.
|
No comments:
Post a Comment