Monday, September 11, 2017

JPM KAMUAPISHA RASMI PROF. IBRAHIM JUMA KUWA JAJI MKUU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo amemuapisha
 Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania, ambaye alimteua kushika wadhifa huo 
Septemba 10, mwaka huu (Jumapili).
Image result for kuapishwa kwa jaji ibrahim juma
Katika ghafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam iliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa wakiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Majaji wengine wa Tanzania, Jaji Ibrahim Juma aliyeapishwa amesema anashukuru kwa kurasimishwa kushika wadhifa huo, ambao alikuwa ana ukaimu takriban miezi nane mpaka alipoteuliwa kuwa Jaji Mkuu.



Katika hotuba yake ya kwanza Jaji Mkuu Ibrahi Juma ameahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa weledi ikiwemo kulinda sheria na kuweka imani kwa wananchi, kwani wao ndiyo watetezi wao.

"Jambo ambalo ni muhimu kwetu sisi katika kufanya kazi ni kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwa na imani ya wananchi, kwa sababu wananchi wasipokuwa na imani na Mahakama pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama hawatakuja kwetu ili kutatua matatizo yao. Sisi tumejiwekea mipango ya kuhakikisha tunaendelea kupata imani ya wananchi wetu, na tutafanya hivyo kwa kuepuka utovu wa maadili, vitendo vya rushwa na ucheleweshaji wa mashauri", amesema Jaji Mkuu Ibrahim Juma.

Ibrahim Juma alianza kutumikia wadhifa wa Kaimu Jaji Mkuu tokea Januari 18 mwaka 2017, baada ya aliyekuwa Jaji Mkuu wa nchi Mheshimiwa Mohamed Chande Othman kustaafu.

No comments: