Tuesday, September 5, 2017

MAMA SAMIA ANOGESHA TAMASHA LA JINSIA MWAKA 2017 ANGALIA HAPA

Leo ikiwa ni tarehe 5 ya mwezi wa 9 Tamasha la 14 la jinsia limezinduliwa rasmi na Makamu wa kwanza wa Rais Mwanamke nchini Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.

Katika uzinduzi huo ulioudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri akiwemo Spika mstaafu wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mama Anna Makinda, Estar Bulaya, Mama Gertrude Mungella, na mabalozi wa nchi mbalimbali pamoja na wadau wa taasisi binafsi kama TAMWA, LHRC, UN Woman na wengine wengi.

Pia kuachilia mbali uzinduzi huo mgeni rasmi Mama Samia Suluhu Hassan alitoa zawadi ya tuzo kwa wanaharakati na wanawake waliofanya vizuri katika ukombozi wa wanawake na kuwa mifano ya kuigwa, kwa wale waliodhuria walipewa zawadi zao papo kwa papo na wale waliofariki au kutoudhuriwa walichukuliwa na wawakilishi wao.

Katika hotuba yake Mama Samia amewapongeza TGNP kwa kuwaleta watu waliofanya makubwa kwa nchi hii na kuona mchango wao mkubwa uliofanywa na watu hao kwani mtu kama Mama Gertrude Mungella, ndiye aliyewatengeneza wao kuona wanawake wanaweza hata na yeye kuthubutu kuona anafaa kuwa kiongozi ndio maana mpaka sasa amekuwa Makamu wa Rais.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Bi. Lilian Liundi akitoa ufafanuzi wa jambo furani katika Tamasha la 14 la Jinsia lililofanyika makao makuu ya mtandao huo Mabibo jijini Dar es salaam.
Aidha aliendele kuipongeza TGNP kwa kuwa inafanya kazi sambamba na serikali na pale serikali inapokosea huambiwa ukweli na kujirekebisha mfano. alimuona kijana wa taasisi hiyo kwenye tv akichambua bajeti na alipenda vile alivyokuwa akielezea vizuri sana.

Lakini pia serikali kushirikiana na taasisi binafsi inafanya jitihada za kuhakikisha inamkomboa mwanamke kutoka kwenye mifumo kandamizi na kumleta kwenye maendeleo endelevu ifikapo 2030 kama inavyosema mikataba ya kimataifa na ya kikanda ambayo serikali imeingaia.

Uwezeshaji wanawake kiuchumi pia ni miongoni mwa malengo ya serikali ndio maana ilianzisha benki ya wanawake ambayo ilishindwa kuendelea kutokana na changamoto mbalimbali, lakini kwa sasa wako mbioni kuifufua kwani ndiyo iliyowafanya wao kupewa zawadi na Umoja wa Afrika AU kwa kuona wako vizuri katika uwezeshaji wanawake.

Na katika jambo lingine serikali imetoa asilimia 30 ya zabuni zake kwa ajiri ya wanawake wenye uwezo wa kuizungusha ili zilete matunda mazuri na kwa kila halmashauri kwenye mapato yake itoe asilimia 5 kwa ajiri ya mifuko ya wanawake ili waweze kujiendeleza kiuchumi.

Na mwisho Mama Samia aliwaomba wazazi kuwapeleka watoto wao mashuleni kwani elimu ndio msingi wa maisha na waachane na mila potofu za mtoto akimaliza darasa la saba aolewe kwani serikali kuona kuwa sekondari ni gharama imeamua kufata ada ili mtoto apate elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.


Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt akisalimia wageni waalikwa kwenye Tamasha la 14 la Jinsia lililofanyika makao makuu ya Mtandao wa Jinsia (TGNP)

Katibu Mkuu Wizara Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bi. Siaba Nkinga akitoa neno kwa wageni waalikwa, na kumkaribisha makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassani akitoa elimu ya kupinga  ukatili wa kijinsia kwa  wageni waalikwa katika Tamasha la 14 la Jinsia lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia TGNP mapema leo jijini Dar es salaam.

Muimba mashahiri mashuhuri Bi. Subira Kibiga akiimba shairi kwa ustadi mkubwa mbele ya mgeni rasmi Mh. Mama Samia Suluhu Hassani kwenye uzinduzi wa Tamasha la 14 la Jinsia lililofanyika Mabibo jijini Dar es salaam.

Kikundi cha ngoma kikitumbuiza mbele ya mgeni rasmi Mama Samia Suluhu Hassa katika Tamsha la jinsia la 14 lililofanyika makao makuu ya Mtandao wa Jinsia TGNP Mabibo jijini Dar es salaam.

Mgeni rasmi Mama Samia Suluhu Hassani akimpa tuzo Mama Anna Makinda kwa kuwa spika wa kwanza mwanamke wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Tamasha la 14 la Jinsia lililofanyika Mabibo Dar es salaam.

Mgeni rasmi wa Tamasha la 14 la Jinsia Mama Samia Suluhu Hassan akimpa tuzo Mama Gertrude Mungela kwa mchango wake wa ukombozi wa mwanamke kimapinduzi katika tamsha hilo lililofanyika mapema leo jijin Dar es salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya bodi ya TGNP Mtandao Bi. Vicensia Shule kushoto akijaribu kuandika  baadhi ya vitu kwenye Tamasha la jinsia mwaka 2017, pembeni ni makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassani kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara Afya Jamii Maendeleo Jinsia Wazee na Watoto Mh. Siaba Nkinga wakipewa elimu juu ya kilimo cha mboga kisichochukua eneo kubwa na wataalamu wa kata ya Kipunguni.

Mama Samia Suluhu Hassani akisain daftari la wageni alipotembelea banda la TAMWA baada ya kuzindua rasmi Tamasha la 14 la Jinsia lililofanyika mapema leo jijini Dar es salaam

No comments: