Baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakidai vyombo vya usalama kutoka nje ya nchi vije kufanya uchunguzi wa shambulio la MbungeTundu Lissu, Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbaas amefunguka na kuhoji watu wangapi wamekufa na wazungu hawakuja.
Kupitia ukurasa wake wa twitter Dkt. Abbas amehoji kwa kuandika "Waje wazungu? Wamekufa watu wangapi Kibiti hatukuita wazungu?Lakini hatujui pia hata hao wazungu kwao makosa ya jinai pia yamewazidi nguvu?
Hata hivyo Dkt Abbas ameongeza kwamba tabia ya kutuhumiana kunapotokea kosa la jinai ambalo limetendwa kwa mtu yoyote au mwanasiasa siyo vizuri kwani kufanya hivyo kunakufanya uwe mshukiwa namba moja wa tukio.
Ameongeza kwamba kwamba ni "busara vyombo vya dola vikaachwa vifanye kazi yake kwanza na siyo kutuhumu".
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia viongozi wake wamekuwa wakitaka serikali iruhusu vyombo vya kimataifa waje nchini kufanya uchunguzi juu ya shambulio la Tundu Lissu aliyepigwa risasi na waru wasiojulikana Septemba 7 akiwa nje ya nyumba yake Area D' Dodoma alipokuwa akitokea bungeni mchana.
No comments:
Post a Comment