****
Mbunge wa Singida Mashariki, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, na rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)Tundu Lissu leo mchana Alhamis Septemba 7,2017 amepigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Dodoma na inaelezwa kuwa hali yake ni mbaya.
Tundu Lissu amepelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa ametoka bungeni na kwenda nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha mchana.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.
Akizungumza na kituo cha ITV Mwenyekiti wa CHADEMA Freeaman Mbowe amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo
Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari, huku wengine wakilia.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Charles Kihologwe amewataka watu hao kukaa mbali na chumba cha upasuaji lakini wengi wanakataa wakisema hawamwamini mtu yeyote.
Asubuhi, Lissu alihudhuria kikao cha Bunge na aliomba mwongozo wa Naibu Spika akihoji kuhusu taarifa za kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na almasi kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu badala ya kujadiliwa na Bunge kwanza.
TAARIFA ZA JIONI HII ZINAELEZA KUWA TUNDU LISSU AMEHAMISHIWA KWENYE HOSPITALI YA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI
Mbowe akiwa na Dereva wa Tundu Lissu aliyeshika nguo zenye damu
Dereva wa Tundu Lissu
Gari la Tundu Lissu alilokuwa nalo
Matundu ya risasi katika gari
No comments:
Post a Comment