Ili kwenda sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya
kuwa na uchumi wa viwanda Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Poul Makonda ameeleza
jitihada wanazozifanya ili kufikia malengo hayo.
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo mkuu wa mkoa huyo
alisema kuwa serikali ya mkoa wa Dar es salaam inafahamu kuwa kuna viwanda zaidi
ya 2000 na katika viwanda hivyo kuna makundi 3 ambayo ni viwanda vikubwa, vya
kati na viwanda vidogo.
Lakini wao wameamua kuwekeza katika viwanda vidogo ili
viweze kuongezeka kufikia kuwa viwanda vya kati na hatimaye kuwa viwanda
vikubwa, na ufanikishaji wa hili utaanza hivi karibuni kutokana kwamba
wameshaongea na NSSF kuweza kuwekeza katika viwanda hivi.
Na pia Mh Makonda alisema kuwa kila halmashauri imetakiwa kutenga
asilimia 10 kwa ajiri ya wazee, wakina mama na vijana, na kwa mkoa wa Dar es
salaam ambao una halmashauri 5 hivyo kuna takribani bilioni sita zimetengwa kwa
ajiri ya wajasiliamali wadogo na wao wanachotakiwa kukifanya ni kuleta
michanganuo ya biashara zao katika ofisi ya mkuu wa mkoa na kupata fedha hizo
zenye riba nafuu.
Aidha mkuu wa mkoa huyo aliongeza kwa kusema wajasiriamali
wadogo watapata nafasi ya kuuza bidhaa zao katika maonyesho ya biashara yatakayokuwa
yakifanyika kwa mwezi mara moja katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es
salaam na zitauzwa bidhaa za ndani peke yake na hakutakuwa na bidhaa toka nje.
Lakini pia wamachinga watatakiwa kuuza bidhaa zinazozalishwa
hapa kwetu ambazo zinatoka katika viwanda vyetu kwani hii itasaidia kukuza soko
la ndani na kuongeza wigo wa ajira kwa vijana wa hapa nchini kwetu.
No comments:
Post a Comment