ILI kufikia uchumi wa kati na wa viwanda
Serikali imeshauriwa kutowaacha wanawake nyuma ambao ndio kundi kubwa la
Watazania wote kwa asilimia zaidi ya 51 kwa mujibu wa sense ya mwaka 2012.
Wito huo
umetolewa na Mratibu wa programu ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Care,
Mary Ndaro, katika mjadala wa wazi kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017
ambalo ni mara ya 14 linafanyika tangu lianzishwe.
Alisema ili nchi yoyote iweze kuendelea
kiuchumi, kiutamaduni na kijamii inatakiwa iende na wananchi wake wote na sio
idadi fulani ya watu hivyo kwa Tanzania ambayo ina wanawake zaidi ya asilimia
51 ili iweze kuendelea lazima isiwaache nyuma wanawake hao ambao ndio wengi
zaidi ukilinganisha na wanaume.
Alisema hali hiyo haimaanishi kwamba
wanaume waachwe nyuma lakini ni muhimu kama inataka kuendelea lazima isiwaache wanawake
kwa kuhakikisha ardhi inaongelea masuala ya wanawake ambayo kwa sasa inampa fursa
ya kutumia tu bali imwezeshe kumiliki, kutumia na kufanya maamuzi kwenye vyote
vitokana navyo na ardhi.
“Hapo tu ndipo tutapata nafasi ya kuongelea
maendeleo, Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati lakini tukiacha hawa wananchi
ambao ni wengi tutakuwa tunapiga makitamu,” alisema Mary.
Alisema kwa upande wa sera ya ardhi
wanapokuwa wanazungumzia masuala mtambuka hakuna sehemu yoyote inayoonesha neno
jinsia, pia inaongelea wanawake kutumia na sio kumiliki.
“Kwahiyo tuna jukumu la kuhakikisha sera na
sheria zetu hazimfanyi mwanamke kuwa ili aweze kumiliki fursa za kiuchumi lazima
aungane na mwanaume kwasababu si wanawake wote wenye wanaume pembeni wa
kuwashikiria.
Mwanaharakati Mkongwe nchini, Dk Getrude Mongela akisisitiza jambo kwenye mjadala wa wazi katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017. |
“Kupitia sualala ardhi tunaona ni muhimu
kuhakikisha sera inaenda mbele zaidi ya fursa wanawake kutumia kwasababu
tumepewa hizo fursa miaka mingi iliyopita ukilinganisha tangu Tanzania ipate
uhuru yapata miaka 56.
“Imetosha kusema kuwa kidogo kidogo
wanawake watasogea wakati wa kusogea ni sasa kwani karibu asilimia 70 ya
wanawake Tanzania ardhi inawahusu haijalishi wa kijiji au mjini na kama
tunaongelea ukombozi wa kiuchumi lazima tuongeleea ardhi kwa mlengo wa kijinsia,”
amesema Mary.
Mwanachama wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP), Profesa Marjorie Mbilinyi,akiuliza swali kwa watoa mada kwenye mjadala wa wazi katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017.
|
No comments:
Post a Comment