Serikali ya
jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chombo chake muhimu cha kutunga sharia kinachofahamika
kama bunge, linapotengeneza bujeti yake limeshauriwa kuwa bajeti hiyo iwe na mlengo
wa kijinsia
Muwezeshaji wa TGNP Mtandao mama Gemma Akilimali akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika Tamasha 14 la Jinsia lililoandaliwa na Mtandao wa jisia TGNP |
Hayo yamesemwa mapema leo na mwanachama wa TGNP Mtandao Mama Gemma. S. Akilimali alipokuwa akiwasilisha mada hiyo katika Tamasha la 14 la Jinsia linaloendelea kufanyika makao makuu ya mtandao huo.
“Tunapozungumzia
bajeti ya kijinsia ni ile bajeti isiyo na upendeleo kwa upande wowote bali
iangalia na itoe nafasi kwa watu wenye mahitaji maalum kama walemavu na kuwapa
fursa sawa wanawake kwa wanaume, lakini pia kutoa upendeleo kwa kundi linaloathirika
zaidi kwenye vipaumbele kama elimu, maji, afya nk”. alisema Gemma
Lakini pia Mama
Gemma alisema kuwa TGNP Mtandao ndilo shirika la kwanza kwa afrika kuanza kupigia
kelele bajeti yenye mlengo wa kijinsia, na ndilo shirika lililofundisha
mashirika mengi katika bara la afrika na mashirika hayo kwa sasa yameweza
kufanikiwa kuwa na bajeti hiyo lakini kwa Tanzania bado hatujaweza kufikia kuwa
na bajeti ya aina hiyo na baadhi ya nchi hizo ni kama Nigeria, Uganda nk.
Baadhi ya wawasilishaji mada wakiwa makini kufuatilia mjadala unaoendeshwa na Mama Gemma Akilimali katika Tamasha la 14 la Jinsia |
Aliendelea
kusema kipindi wao wanaanza kudai bajeti yenye mlengo wa kijinsia, serikali
ilikuwa ikitengeneza bajeti kwa siri sana kiasi kwamba wananchi hawajui kiwango
gani kimewekwa kwenye elimu au afya na jambo lingine kwamba ile pesa ikitoka
wizara ya fedha kwanda wizara ya afya au elimu kunawatu waliopo kati hapo
wanaipunguza na kutoka wizara husika mpaka kwenye mradi inaibiwa tena kiasi
kwamba inayofika kwenye mradi inakuwa ni kidogo sana na inashindwa kumudu
mahitaji husika.
Na pia
katika utengenezaji wa bajeti haukuwa na uwiano sawa, ilikuwa wanapanga wanaume
peke yake na kutowapa fursa wanawake ya kushiriki katika majadiliano wala maamuzi
na wizara ilipoulizwa katika hali ilisema kazi hii huwa inafanywa mpaka usiku
hivyo sio vyema kwa wanawake kuwepo mpaka muda huo. Wakati kwenye upangaji huo
kunakuwa na posho hivyo inamfanya mwanamke kukosa fedha hiyo ambayo ingemsaidia
na yeye kupunguza majukumu yake.
Kutokana na
hili wao wakiwa kama watetezi wa bajeti yenye mlengo wa kijinsia waliomba
wizara ya fedha kufanya utafiti mdogo ambao nao pia uliibua changamoto kama
zifuatazo, viwandani wanawake wanapewa nafasi zile ndogo ndogo kama kupanga
nguo, kufagia na nafasi za juu kama wakurugenzi na nyinginezo wanapewa wanaume.
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika leo ikiwa ni siku ya tatu ya Tamasha la jinsia lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia TGNP |
Na eneo la pili lilikuwa ni kilimo ambapo kulikuwa na shida
kwa kuwa mwanamke mazao yake anayovuna yanatumika kwenye chakula nyumbani,
lakini mwanaume yeye akivuna anaenda kuuza na kuingiza pesa hali ambayo
inamyonya huyu mwanamke na kumfanya asiendelee mbele.
Lakini swala lingine pia ni mapato na matumizi ya serikali na
hii inasimamiwa na ulipaji wa kodi lakini cha ajabu kwenye kulipa kodi
anaumizwa mwananchi wa chini ambae hana chochote analazimishwa kilipa kodi na
wakati makampuni makubwa ya migodi inapewa miaka 5 ifanye kazi bila kulipa
chochote,
lakini pia misamaha
inayotolewa kwa makampuni na hoteli kwa mfano muwekezaji wa hoteli akija nchini
anapewa miaka mitano ya kufanya kazi bila kulipa kodi na akiona miaka hiyo inakaribia
kuisha anabadilisha jina ili kukwepa kodi mfano. Kilimanjaro Kempinsky
iliyobadilishwa na kuitwa HYTTE Regency au Sheratoni ambayo sasa ni Dar es
salaam Serena.
No comments:
Post a Comment