Saturday, September 2, 2017

Tiketi za ‘Tigo Fiesta 2017 - Tumekusomaa’ Zaanza Kuuzwa Kupitia TigoPesa.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko Tigo, William Mpinga, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu namna ya kununua tiketi za Tigo Fiesta 2017 kwa njia ya Tigo Pesa. Kulia ni Mratibu wa Tigo Pesa, Daniel Mmbaga. (Na Mpiga Picha Wetu).

Tiketi za mapema zinapatikana kwa mitandao yote kwa 10% punguzo  la bei


Dar es Salaam,  Jumamosi  2 Septemba, 2017- Tigo inatoa punguzo la asilimia 10% kwa wateja wote watakaonunua tiketi zao za msimu wa Tigo Fiesta 2017 Tumekusomaa kupitia huduma ya Tigo Pesa.

Akizindua mauzo ya tiketi za Tigo Fiesta 2017 kupitia njia ya mtandao jijini Dar es Salaam leo, Mtendaji Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Tigo, William Mpinga aliwashauri wapenzi wa Tigo Fiesta kuchukua fursa hii kupata tiketi zao kwa TZS 9,000/- tu, hii ikiwa ni punguzo la 10% ya bei kupitia TigoPesa, au mtandao wowote wanaotumia kwa sasa. Bei halisi ya tiketi getini itakuwa ni TZS 10,000/-.  

Tigo ndio kampuni ya kwanza kuwezesha wateja kutuma pesa kwa njia ya mtandao kwenda mitandao mingine nchini. Kwa moyo huo huo, Tigo sasa inawapa wateja wa simu wanaotumia mitandao mingine nchini kununua tiketi za Tigo Fiesta 2017 kupitia mitandao yao.

‘Kununua tiketi ni rahisi. Fuata utaratibu wa kawaida wa kutuma pesa na tuma TZS 9,000 kwenda namba ya TigoPesa 0678 888 888. Hapo hapo utapokea ujumbe mfupi wa SMS unaothibitisha manunuzi yako ya tiketi. Hifadhi huo ujumbe mfupi. Baadaye utapokea maelekezo ya jinsi na wapi pa kwenda kuchukua tiketi yako,’ alisema.

‘Tigo inajiandaa kutoa ofa nyingine kibao katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2017 kwa hiyo wateja wetu wa Tigo, watumiaji wa TigoPesa na wapenzi wote wa Tigo Fiesta 2017 wakae tayari kufurahia ofa hizi bomba kadri ya tutakavyokuwa tunazitangaza.,’ Mpinga aliongeza.

Mwaka huu msimu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa utajumuisha mikoa ya Arusha Kahama, Musoma, Mwanza, Tabora na Dodoma. Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa pia itatua katika mikoa ya Iringa, Songea, Njombe, Sumbawanga, Morogoro, Tanga, Moshi na Mtwara, kabla ya kuhitimishwa jijini Dar es Salaam.

No comments: