Wakulima kote
nchini wametakiwa kutumia mbolea asili za samadi na kuepukana na matumizi ya mbolea
za viwandani kwani sio nzuri kwa afya ya watumiaji japokuwa tunziona nzuri kwa
kuwa mazao yanakuwa kwa muda mfupi.
Akiongea na
wakulima kutoka mikoa mbalimbali ya hapa Tanzania katika warsha iliyoandaliwa
na Mtandao wa Jinsia TGNP muadhiri wa chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Bw. Boniphace Cija alisema inabidi kuachana nayo ikiwezekana kupunguza matumizi yake.
Bw. Boniphace
ameshauri kwa wale wenye mashamba makubwa vyema kutumia kilimo Mseto(mixed farming) ambacho kinahusisha mifugo na mimea kuwa kwa pamoja, hii
itasaidia kupata samadi kwa urahisi na kuachana na mbolea za viwandani.
Na tena
itasaidia kutokana kwamba mabaki ya mimea yatatumika kama chakula kwa mifugo na
samadi ya mifugo itatumika kwa ustawi wa mimea hivyo kuepuka tatizo hilo la kula
mboga ama matunda yasiyo na virutubisho asili.
Muadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine Bw. Boniphace Cija akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika warsha ya kilimo iliyoandaliwa na TGNP Mtandao mapema leo jijini Dar es salaam. |
Lakini pia
swala lingine ni kutumia dawa za kuulia wadudu wanaokula mazao ya mimea pia ni
tatizo kwani sio wadudu wote ni wabaya hivyo kuna baadhi ya wadudu wanahitajika
kwa ajili ya virutubisho kwenye udongo.
Endapo kutatokea
tatizo la ugonjwa kwa mimea suluhu sio kupiga dawa unaweza kutumia kilimo cha Mzunguko wa Mazao kwani kinasaidia kuondoa magugu kwenye shamba lakini pia
kuondoa magonjwa ya mimea na kuboresha viumbe hai muhimu katika udongo.
Na kilimo
hiki ufanyika kwa mazao tofauti kulimwa katika shamba moja katika msimu
tofauti ama vipande tofauti. Mfano mimea inayopunguza virutubisho kama nitrogen(jamii
ya nafaka) itanguliwe na ile inayoongeza nitrogen katika udongo( jamii ya
mikunde).
Lakini pia
kilimo hiki upunguza athari ya mmomonyoko wa ardhi na kuboresha rutuba ya
udongo na kusaidia kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao.
Na kitu
kingine magugu au wadudu wanapokuwepo shambani kwako sio vyema kupiga dawa au
kuchoma moto kwani kufanya hivyo ni kuharibu ardhi kwa kuondoa rutuba na
kuunguza wadudu wanaorutubisha udongo, unachotakiwa kukifanya ni kumwaga samadi
nyingi ili kuua vimelea wabaya na magugu.
Kwani kwa
kuchoma sio tu kuharibu ardhi lakini pia unasababisha madhara hata kwa viumbe
wengine kutoweka kwenye ardhi ambao wapo kwa ajili ya kurutubisha udongo, hivyo unashauriwa kutumia njia nyingine mbadala kama kufuga mifugo kama kondoo au bata wanasaidia kula magugu tu hivyo wanazuia magonjwa ya mimea.
No comments:
Post a Comment