Monday, September 4, 2017

WANADAR ES SALAAM KUPIMWA AFYA ZAO BURE KUANZIA TAREHE 6

Watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upimaji wa afya bure wa magonjwa yote yanayoambukiza na yasiyoambukiza litakalofanyika viwanja vya Mmnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Poul Makonda akiongea na waandishi wa habari kuhusu zoezi la upimaji wa magonjwa yote bure linalotarajiwa kuanza tarehe 6 mwezi huu mnazi mmoja  jijini Dar es salaam.
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Poul Makonda amesema watanzania waje kwa wingi kwani hakutakuwa na malipo yoyote na zoezi litadumu kwa siku tano kuanzia jumatano ya tarehe 6 mpaka jumaapili ya tarehe 10 kanzia asubuhi na kuendelea.

Pia mkuu wa mkoa huyo alipenda kuwashauri watanzania kuwa na utaratibu wa kupima afya zao ili kuweza kujikinga na kutumia dawa sambamba na ugonjwa ulionao, na pia aliwataka waje watu wa lika zote vijana, wazee na hata watoto kwani siku hizi magonjwa hayachagui umri.
Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bi. Grace Magembe akiongea na waandishi wa habari kuhusu zoezi la upimaji wa magonjwa yote bure, zoezi linalosimamiwa na ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam.
Na katika zoezi hilo watakuwepo madaktari zaidi ya 200 kutoka hospitali mbalimbali za jiji la Dar es salaam zikiwemo za  serikali pia za watu binafsi zilizoamua kuunga mkono zoezi hilo kama Muhimbili, Amana, Mwananyamara, Aghakhan, TMJ, Regency n.k na pia magonjwa yote yatapimwa mahali kama kisukari, kansa, tezi dume, meno, macho

Aidha amezipongeza Hospital na zilizomuumga mkono ikiwemo Muhimbili, Ocean Road, Amana, Temeke, Mwananyamala, Muhimbili, TMJ, Sanitas, Agha Khan, Regency, Kairuki, TANCDA, IMMI Life, APHTA, CCP Medicine, MDA, NHIF, Wandile wa kaya, P Consult, Besta Diagnestics, Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, Jamii Bora na Damu salama.


No comments: