Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori akizungumza wakati wa uzindulizi mradi wa usambazaji majisafi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), katika eneo la Kilungule B. Zaidi ya wakazi 5000 wanatarajia kunufaika na mradi huo. Kutoka kushoto ni Meneja wa DAWASCO - Kimara, Paschal Fumbuka na Kulia kwa Mkuu wa Wilaya ni Diwani wa Kata ya Kimara, Paschal Manota.
Diwani wa Kimara, Paschal Manota akizungumza wakati wa uzindulizi mradi wa usambazaji majisafi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), katika eneo la Kilungule B. Zaidi ya wakazi 5000 wanatarajia kunufaika na mradi huo. Kutoka kushoto ni Meneja wa DAWASCO - Kimara, Paschal Fumbuka na Kulia kwa Mkuu wa Wilaya ni Diwani wa Kata ya Kimara, Paschal Manota.
Meneja wa DAWASCO - Kimara, Paschal Fumbuka akitoa ufafanuzi juu ya mradi huo ambao umezinduliwa leo eneo la Kilungule B, ambapo walikuwa hawakuwahi kuipata huduma hiyo kwa miaka 20. Aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo ni moja ya hatua zinazofanywa na Dawasco Mkoa wa Kimara katika kuondoa kero ya ukosefu wa huduma ya Maji katika maeneo yasiyo kuwa na huduma hiyo kwenye Mkoa huo.
Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori akiwa ameongozana na Diwani wa Kimara, Paschal Manota na Meneja wa Dawasco - Kimara, Paschal Fumbuka pamoja na wananchi wa eneo la Kilungule B kuelekea kuzindua mradi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori pamoja na Diwani wa Kimara, Paschal Manota wakizindua mradi wa usambazaji majisafi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), katika eneo la Kilungule B. Zaidi ya wakazi 5000 wanatarajia kunufaika na mradi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori pamoja na Diwani wa Kimara, Paschal Manota wakifurahia.
Majiiiiiiiiiiiiiiiiii hayo...
Akina mama wakifurahi maji.
Maneja akitoa neno la shukrani mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.
Wakazi wa Kilungule B wakichota maji mara baada ya zoezi la uzinduzi kufanyika.
Wananchi wakijiandisha ili waweze kupimiwa maeneo yao wapatiwe maji.
No comments:
Post a Comment