Tuesday, October 31, 2017

TIGO WAZINDUA KAMPENI MPYA YA TUMEKUSOMA



Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma wa kampuni ya Tigo, David Umoh, pamoja na Mtaalam wa Huduma kwa Wateja, Kitengo cha Biashara, Sarah Cyprian wakizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni mpya ya Tumekusoma inayoendana na uzinduzi wa namba mpya ya huduma *147*00#.  Namba *147*00#  itawawezesha wateja wa Tigo kupata huduma mbali mbali za sauti na VAS kutoka Tigo kwa hatua rahisi zaidi, pamoja na kupata bonasi kubwa ya vifurushi na muda wa maongezi kila watakapotumia namba hiyo mpya.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandhishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa Kampeni mpya ya 'TUMEKUSOMA' inayokwenda sambamba na uzinduzi wa namba mpya ya huduma za Tigo (*147*00#) itakayowawezesha wateja wake kupata huduma mbalimbali kwa urahisi zaidi, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kampuni hiyo, Makumbusho jijini Dar es sa salaam.





Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania, leo imezindua rasmi kampeni mpya ya Tumekusoma, ambayo ni mkakati mkubwa wa kufikia wateja wake na bidhaa na huduma bora zinazoendana na mahitaji yao kwa muda muafaka. Kampeni hii ya Tumekusoma pia inaendana na uzinduzi wa namba mpya ya huduma ya *147*00# itakayowawezesha wateja wa Tigo kupata huduma mbali mbali za sauti na VAS kutoka Tigo kwa hatua rahisi zaidi. Wateja wa Tigo watakaotumia namba hiyo mpya pia watapata bonasi kubwa ya vifurushi na muda wa maongezi kila watakapotumia namba hii mpya.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya Tumekusoma jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Bidhaa na Huduma za Tigo, David Umoh alisema, ‘Tumesoma hitaji la watumiaji wa mitandao ya simu la menu au namba ya huduma ambayo itarahihisha hatua za kununua vifurushi au kufanya miamala ya fedha. Menu hii mpya inajibu mahitaji hayo yote. Ni rahisi sana kutumia. Pamoja na haya, namba mpya ya *147*00# inawapa wateja ofa kabambe ya nyongeza ya muda wa maongezi, SMS na data kila mara watakaponunua vifurushi kupitia namba hii,’ Umoh alisema.
Alibainisha faida nyingine kubwa ya menu hiyo mpya ni ofa za Chapchap, zinazowawezesha wateja kununua muda wa maongezi na vifurushi vinavyoendana na mahitaji na tabia zao za kipekee za matumizi ya simu, jambo ambalo linaendana na lengo la Tigo la kuwaongezea thamani wateja wake. ‘Tumesoma mahitaji ya wateja wetu na kuwapa suluhisho muafaka linaloendana na mahitaji yao ya kipekee kupitia menu hii inayorahisisha matumizi yao ya simu kupitia mtandao wetu ulioboreshwa na uliosambaa kote nchini,’ alisema.

Tigo inaendelea kuwa mtandao unaoongoza kwa kuzindua bidhaa na huduma zinazoendana na mahitaji ya wateja. Tigo ndio mtandao ulioleta mageuzi makubwa zaidi katika mifumo ya bei ya mitandao ya simu za mkononi nchini. Tigo pia ndio iliyokuwa mtandao wa kwanza kuzindua huduma za vifurushi vya sauti na data, ndio mtandao wa kwanza kuzindua simu za kisasa zenye mfumo wa lugha ya Kiswahili na pia ndio mtandao wa kwanza nchini kuzindua huduma ya Tigo Pesa iliyowezesha wateja wake kufanya miamala ya fedha nje ya nchi iliyokuwa na uwezo wa kubadili thamani ya fedha kulingana na thamani ya fedha ya nchi husika.

‘Kupitia Tumekusoma, tunawakaribisha wateja wote wa Tigo wajiunge nasi katika safari hii ya kumbukumbu ya hatua tulizopiga na mafanikio makubwa tuliyopata katika kipindi hiki cha kuwahudumia Watanzania. Tunawakaribisha nyote kuungana nasi katika mageuzi ya kidigitali nchini na kufurahia mtandao wetu wa Tigo ulioboreshwa na uliosambaa kote nchini Tanzania,’ Umoh alisema. Menu mpya iliyoboreshwa ya *147*00# inaanza kufanya kazi leo na wateja wa Tigo wanaweza kuanza kupata bonasi murwa kwa manunuzi yote wanayoyafanya. Tunawakaribisha wateja wetu wakae mkao wa kupokea ofa zaidi kabambe huku tukiendelea katika safari hii ya kuwahudumia wateja wetu kwa urahisi zaidi na kwa ubora wa hali ya juu.

ORODHA YA MAKAMPUNI YA SIMU YALIYOTII AGIZO LA RAIS DKT. MAGUFULI KUJIUNGA NA MFUMO WA E-RCS

Kampuni za Smile Tanzania, Smart na Vodacom ndio kampuni pekee za simu ambazo hazijatii agizo la Mhe. Rais la kujiunga na Mfumo wa Kulipa Kodi Kielektroniki.

ZITTO KABWE ATIWA MBARONI NA JESHI LA POLISI, KAULI YA JPM YAHUSISHWA YA KUWAKAMATA WATOA TAKWIMU ZA UONGO KWA SERIKALI YAKE

Kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amekamatwa na Jeshi la Polisi asubuhi hii  akiwa nyumbani kwake na amepelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Image result for zitto kabwe akamatwa
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa chama hicho, Abdallah Khamis imesema Zitto amekamatwa asubuhi hii Masaki wilayani Kinondoni, akidaiwa kutoa kauli za uchochezi wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi wilayani Temeke juzi.

Pia kukamatwa huko kwa Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini ,kuna kuja ikiwa ni wiki moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuvitaka vyombo vya usalama kuwamata watu wanaotoa takwimu tofauti na serikali yake na kuwachukulia hatua kupitia sheria ya Takwimu ya mwaka  2014 ambayo inatoa hukumu kwenda jela hadi miaka miwili kwa mtu anatoa Takwimu tofauti.

Agizo hilo la Magufuli ambalo alikumtaja jina mtu, lakini wachambuzi wa mambo wanasema kauli hiyo ilikuwa inamlenga Zitto ambaye mara kwa mara amekuwa mkosoaji mkuu wa serikali ya Magufuli kwa kusema hali ya uchumi wa nchi ni mbaya huku akitoa takwimu mbali mbali ambazo zinaonesha hali hiyo ya uchumi.

Monday, October 30, 2017

UNDANI KUHUSU SHEREHE ZA HALLOWEEN KILA IFIKAPO OKTOBA 31


Na Jumia Travel Tanzania

Inawezekana utakuwa umesikia watu au kusoma kwenye mitandao ya kijamii kuhusu sherehe za Halloween lakini ukawa hauelewi. Mbali na hapo inawezekana pia umekutana na matangazo kadhaa yakikutana kushiriki kwenye sherehe za sikukuu hiyo sehemu kadhaa za starehe hususani vilabu vya usiku hapa nchini.
Kutokana na utandawazi uliosababisha dunia kuwa kijiji tumejikuta kwa namna moja ama nyingine tukishiriki matukio mbalimbali kwa wakati mmoja. Baadhi ya matukio hayo huwa hatuelewi maana yake kwa undani zaidi. Kwa mfano, Halloween kwa namna inavyosherehekewa ni kama ina uhusiano na sherehe za kishetani.

Ikiwa sehemu mbalimbali duniani zimeshaanza maandalizi ya sherehe za Halloween ambazo hufanyika kila ifikapo Oktoba 31 ya kila mwaka, Jumia Travel ingependa kukufahamisha juu ya maana halisi ya sherehe hii.  
Japokuwa umaarufu wa sherehe ya Halloween umetokana na nchi ya Marekani lakini ukweli ni kwamba wanahistoria wanaamini sherehe hii ilianzia nchini Ireland na kusambaa nchi za jirani za Scotland, Uingereza, Ufaransa na baadaye sehemu zingine duniani.

Na kudhihirisha kwamba Marekani inasherehekea sherehe hii kikamilifu, inaaminika kwamba ni sherehe ya pili kwa ukubwa wa kibiashara ndani ya mwaka. Katika kipindi hiki takwimu zinaonyesha kwamba wamarekani hutumia zaidi ya dola bilioni 5 kuadhimisha sherehe hii. Na kwa kuongezea robo ya mauzo yote ya peremende au pipi ya mwaka hufanyika ndani ya kipindi hiki nchini humo.
Halloween ina maana gani na kwanini husherehekewa kila ifikapo Oktoba 31 ya mwaka?

Maana halisi ya neno Halloween ni siku ya mkesha wa siku ya watakatifu wote ambayo huadhimishwa kila ifikapo Novemba mosi. Halloween pia ni ufupisho wa neno ‘Allhalloween, All Hallows’ Evening na All Saint’s Eve’ ambapo husherehekewa kila ifikapo Oktoba 31 ya kila mwaka.

Asili ya Halloween ilitokana na sherehe ya ‘Samhain’ iliyokuwa ikiadhimishwa na watu wa kale wa Ireland au ‘Waseltiki’ kama wanavyojulikana.

Samhain ni sherehe ya wapagani wa kiseltiki ikimaanisha ‘Mwisho wa Majira ya Joto’ ambayo huadhimishwa mwisho wa msimu wa mavuno.

Hiki kilikuwa ni kipindi ambacho walikuwa wakiwasha moto kuuzunguka na kisha kuvalia mavazi yanafanana na ya mashetani ili kuepekana na mizimu inayosemekana huwa inarandaranda usiku huo.

Katika karne ya nane, Papa Gregory III alisema kwamba Novemba mosi itakuwa ni siku ya kuwakumbuka watakatifu na wafia dini wote. Na hapo ndipo ‘Siku ya Watakatifu Wote’ ilipoanzia na jioni yake ilikuwa ikijulikana kama ‘All Hallows’ Eve’ na baadaye kuwa Halloween.
Halloween imepata umaarufu mkubwa kadiri muda unavyokwenda na kuwa kipindi cha kufanya biashara kwa wingi ambapo watoto na watu wazima husherehekea kwa kuvalia mavazi ya kuogofya kama mizimu au mashetani na kwenda kuhudhuria sherehe zinazoandaliwa.

Kwanini watu huvalia mavazi ya kuogofya usiku wa Halloween?

Utamaduni ambao umekuwepo kwa miaka mingi katika kusherehekea Halloween ni pamoja na kuvalia mavazi ya kutisha kama mizimu au mashetani.
Washerehekeaji hufanya hivyo kutokana na asili ya sherehe hii ambapo inaamini kwamba katika mkesha wa siku ya Oktoba 31 kuamkia Novemba mosi mashetani, wachawi na mizimu huwa inarandaranda mitaani kusherehekea kuanza kwa msimu wao - kipindi cha majira ya baridi. Inasemekana kwamba huranda mitaani na kuwachezea watu, kuwatisha, kuwadhuru na kuwafanyia hila mbalimbali kadiri wanavyopenda.

Njia pekee kwa watu waliokuwa wanaogopa kutishwa na mizimu hiyo ni kuwapatia vitu ambavyo walikuwa wanavipendelea, mara nyingi huwa ni vyakula vitamu na zawadi nzuri kama vile peremende kwa kuviacha milangoni.

Au, njia nyingine iliyokuwa ikitumika, kwa watu ambao walikuwa wanaogopa, ni kwa kuvalia mavazi kama yao na kisha kurandaranda mitaani, lengo ni kwa mizimu hiyo kutowatambua na kuwafananisha binadamu hao na wenzao.

Je unajiuliza kama usherehekee sikukuu ya Halloween? Kumekuwa na dhana tofauti juu ya sherehe hii ambayo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa zikihusishwa na ushetani na ushirikina. Hii inategemea namna wewe mwenyewe utakavyosherehekea na kwa malengo gani na kama itaathiri vipi imani yako. Kwa makala haya, Jumia Travel inaamini kwamba utakuwa umefahamu machache kuhusiana na sherehe hii ambayo inazidi kushika kasi kadiri miaka inavyokwenda.

KISHINDO CHA MSIMU WA TIGO FIESTA CHAACHA GUMZO MOSHI...

Wasanii Banarba na Gnako wakishiriki uzinduzi wa huduma mpya ya Tigo ya TUMEKUSOMA ambayo ni namba maalum (code number) itakayowawezesha wateja wa Tigo kuingia kwenye menyu na kupata huduma mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Majengo Manispaa ya Moshi usiku wa kuamkia jumatatu.

Msanii Bright akiwa kwenye jukwaa la Tigo Fiesta liliofanyika uwanja wa Majengo Manispaa ya Moshi usiku wa kuamkia jumatatu.

Chege akiburudisha kwenye jukwaa la Tigo Fiesta liliofanyika uwanja wa Majengo Manispaa ya Moshi usiku wa kuamkia jumatatu.

Msanii Bright akiwa kwenye jukwaa la Tigo Fiesta liliofanyika uwanja wa Majengo Manispaa ya Moshi usiku wa kuamkia jumatatu.

Umati wa wakazi wa Moshi wakiwa wanashuhudia burudani iliyokuwa inatolewa na wasanii .

Gigy Money akiwa katika jukwaa la Tigo Fiesta mapema usiku wa kuamkia jumatatu

Jux akiburudisha wakazi wa Moshi mapema usiku wa kuamkia jumatatu katika jukwaa la Tigo Fiesta .

TIGO Fiesta 2017 imefana vilivyo mkoani Kilimanjaro ambapo wasanii mbalimbali wa Bongo fleva wamefanya vilivyo katika viwanja vya Majengo katika Manispaa ya Moshi kwa kutoa burudani ya kukata na shoka kwa wakazi wa manispaa hiyo.
Katika kuhakikisha kuwa kila mkazi wa Moshi anafurahia vilivyo tamasha maalumu la Tigo Fiesta 2017 ambapo mdhamini mkuu wa tukio hilo la aina yake Tigo Tanzania leo wametangaza namba maalumu ya wateja ambayo ni *147*00# hii inajulikana kama TUMEKUSOMA ambayo  wateja wataweza kufanya kuitumia katika huduma mbalimbali za Tigo.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika tamasha maalumu la Tigo Fiesta 2017 katika Manispaa ya Moshi, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo Tanzania, William Mpinga alifafanua kuwa, namba hiyo mpya (Code number) itatumika kwa wateja wa Tigo kote Tanzania katika kupata huduma mbalimbali za mtandao huo.

Tofauti na matukio  yaliyotangulia, washiriki wote kutoka mtandao wowote kwa tamasha la mwaka huu mbali na kupata huduma ya kulipia kiingilio kwa huduma ya Tigo-Pesa, pia wamepata burudani kabambe kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki kutoka Tanzania.
Wasanii waliotumbuiza katika Tigo Fiesta katika viwanja vya Majengo katika Manispaa ya Moshi ni pamoja na Rich Mavoko, Chege, Nandy, Maua, Vanessa, Jux, Ben Pol, Rostam, Weusia, Darassa,Lulu Diva, Rosa Lee, Mimi Mars, OMG, Gigy Money,  Asley na wasanii wengineo.

Jukwaani Msanii Rosa Ree aliingia kama Malkia na kiti chake nakuwafanya mashabiki wapagawe na wimbo wake Mchagamchaga na nyingine,
Msanii Aslay kama ilivyokawaida yake mashabiki waliweza kuimba nae mwanzo mwisho wa nyimbo zake zote, wimbo wake mhudumu ndio uliwapagawisha zaidi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya kaskazini, Henry Kinabo amewataka watanzania kutumia huduma mbalimbali zitolewazo na Tigo kwa kuwa faida inayotokana na huduma inasasaidia huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo elimu, afya na nyinginrezo ikiwamo mtandao wa intaneti.

“Nawashauri watanzania wote kutumia huduma mbalimbali bora zitolewazo na Tigo  kwani sehemu kubwa ya faida tunayopata tunairudisha kwa jamii kupitia huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu hasa huduma ya intaneti kwashule mbalimbali, mbali madawati tuliyoto mwaka jana..” alifafanua Kinabo. 

JUA KILICHOJIRI KATIKA SOKO LA HISA KWA WIKI ILIYOPITA

Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa kwa wiki iliyoisha Ijumaa tarehe 27 Oktoba 2017.

Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity)
Thamani ya mauzo ya hisa imepungua kutoka Shilingi Billioni 23 ya wiki iliyoishia 20 Oktoba 2017 hadi Shilingi Bilioni 20 kwa wiki iliyoishia 27 Oktoba 2017,
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepungua kutoka hisa Mil 2.8 ya wiki iliyoishia 20 Oktoba 2017 hadi hisa Mil 1.6 ya wiki iliyoishia 27 Oktoba 2017.
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:
TBL…………………………………………99%
SWISS………………………………………0.4%
NMB………………………………………….0.2%
Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umepungua kwa Shilingi Bilioni 432 kutoka Shilingi Trilioni 20.9 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 20.5 wiki iliyoishia tarehe 27 Oktoba 2017. Punguzo hilo limetokana na kupungua kwa bei za hisa za ACA(13%), KA (9%), TTP (8%), EABL (2%) na DSE (2%).
Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepungua kwa Shilingi Bilioni 2 kutoka Trilioni 10.165 hadi kafika Shilingi Trilioni 10.163 wiki hii. Hii ni kutokana na kupungua kwa bei ya hisa za TTP (8%) na DSE (2%).
Kampuni
27 October 2017            (Shilingi)
20 October 2017            (Shilingi)
Badiliko (%)
CRDB
                                  170
                                  170
0.00%
DCB
                                  385
                                  385
0.00%
DSE PLC
                               1,200
                               1,220
-1.64%
MBP
                                  600
                                  600
0.00%
MCB
                                  500
                                  500
0.00%
MKCB
                                  890
                                  890
0.00%
MUCOBA
                                  400
                                  400
0.00%
NMB
                               2,750
                               2,750
0.00%
PAL
                                  470
                                  470
0.00%
SWALA
                                  500
                                  500
0.00%
SWIS
                               3,500
                               3,500
0.00%
TBL
                             13,900
                             13,900
0.00%
TCC
                             15,600
                             15,600
0.00%
TCCL
                               1,200
                               1,200
0.00%
TOL
                                  780
                                  780
0.00%
TPCC
                               1,520
                               1,520
0.00%
TTP
                                  600
                                  650
-7.69%
VODA
                                  850
                                  850
0.00%
YETU
                                  600
                                  600
0.00%
Kampuni zilirodhodheshwa kutokea Masoko mengine



ACA
                               5,460
                               6,290
-13.20%
EABL
                               5,310
                               5,410
-1.85%
JHL
                             10,490
                             10,500
-0.10%
KA
                                  120
                                  110
9.09%
KCB
                                  820
                                  830
-1.20%
NMG
                               2,380
                               2,360
0.85%
USL
                                    80
                                    80
0.00%




Mtaji Jumla Makampuni yote (Bilioni)
                             20,455
                             20,887
-2.07%
Mtaji Jumla Makampuni ya Ndani (Bilioni)
                             10,163
                             10,165
-0.02%
Kiashiria cha DSEI (pointi)
                               2,124
                               2,172
-2.21%
Kiashiria cha TSI (pointi)
                               3,876
                               3,904
-0.72%

Viashiria (Indices)
Kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimeshuka kwa pointi 48 kutoka pointi 2,172 hadi 2,124 pointi hii ikiwa ni kutokana na kushuka kwa bei za hisa za Acacia (ACA) kampuni Kenya Airways (KA), Tetepa (TTP) East African Breweries Ltd (EABL) na Dar es Salaam Stock Exchange Plc (DSE).
Pia kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepungua kwa pointi 27 kutoka pointi 3,904 hadi pointi 3,876 kutokana na kushuka kwa bei za hisa za Tatepa na DSE Plc
Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) kimepungua kwa pointi 1 kutoka pointi 5,380 hadi pointi 5,379
Kiashiria huduma za kibenki na kifedha (BI) kimeshuka kwa pointi 1 kutpka pointi 2,498 hadi pointi 2,497.
Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 2,462
Hati Fungani (Bonds)

Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 27 Oktoba 2017 yalikuwa Shilingi Milioni 500 kutoka Shilingi Bilioni 13 wiki iliyopita ya 20 Oktoba 2017

Mauzo haya yalitokana na hatifungani saba (7) za serikali na mashirika binafsi zenye jumla ya thamani ya Shilingi Milioni 600 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Milioni 500