Ikiwa imebakia siku moja kuanza kusikilizwa tena kwa kesi ya mauaji ambayo inamkabili, msanii Elizabeth Michael (Lulu) amesema yupo tayari kukabiliana na kesi hiyo, ambayo alijua ipo siku itarudi tena.
Lulu ameyasema hayo leo alipokuwa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa alikuwa na taarifa ya kesi hiyo kabla watu hawajaipata kwenye mitandao, na utaratibu wa kisheria ulifuatwa.
“Unajua watu hawajui sheria, kesi haikuwahi kuisha ni pocedure ya kawaida ya mahakama imefuatwa na ni muda wake umefika sasa , siyo kama imeibuka tu, na kwasababu mimi ndiye muhusika nimepata taarifa kwa njia ya kisheria siyo kama nyie kwenye mitandao, na pengine niliipata kabla yenu”, amesema Lulu.
Lulu ameendelea kusema kwamba kuwepo kwa kesi hiyo kunamuathiri kwa kiasi kikubwa kwenye kazi zake na maisha yake kiujumla.
Kesi inayomkabili muigizaji huyo wa bongo movie inatarajia kusikilizwa tena kesho Oktoba 19, 2017 baada ya kuwa nje kwa dhamana kwa muda mrefu.
Elizabeth Michael (Lulu) anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo bila kukusudia cha aliyewahi kuwa muigizaji wa filamu nchini, Steven Kanumba, mnamo April 7, 2012 .
No comments:
Post a Comment