Leo tarehe
18 ya mwezi octoba ni ufunguzi wa semina ya siku tatu iliyoandaliwa na TGNP
Mtandao kwa lengo la kuwakutanisha wafanya biashara wanawake wa mipakani pamoja
na maafisa mbalimbali wanaofanya kazi kwenye mipaka ili kuweza kuzijadili
changamoto zinazowakabili wanawake hao na namna ya kuzitatua.
Katika semina
hiyo iliyowakutanisha washiriki zaidi ya 35 wakiwemo wafanya biashara wanawake
wa mipakani na wadau wa asasi mbalimbali za kiraia na maafisa wa serikali kama
TRA, TBS, SIDO, TWCC na wengine wengi.
Akiongoza semina
hiyo kwa wanawake wafanyabiashara wa mipakani Beatrice Hazekiel alisema lengo
ni kujengeana uwezo na uelewa wa dhana muhimu za jinsia na kuhakikisha mipakani
wanapofanyia shuguli zao kuwe na uwiano sawa wa kijinsia kati ya wanaume na
wanawake katika maamuzi na mambo mbalimbali yanayohusu jinsia.
Lakini pia
muwezeshaji alisema ili kuweza kuwa na usawa wa kijinsia ni lazima watu
kuondoakana na dhima potofu ya mfumo dume ambao unatumika kuwanyanyasa wanawake
na wananchi walio wanyonge katika taifa letu na kuonekana kuwa baadhi ya watu
kuwa ni wanathamani kushinda wengine hivyo kuwanyonya wanyenge hao.
Muwezeshaji huyo
aliendelea kwa kusema kuwa mfumo dume unajengeka au kulindwa na makuzi yetu na
wanawake wengi huona kama ni wakosaji na hawakuwa wanastaili kuwepo walipo kwa
kuona ni makosa yao wenyew lakini sio makosa yao ila ni makuzi toka walipoanza
kukua na kujengewa mfumo wa kuwa wewe ni mtoto wa kike majukumu yako ni kupika
kuosha vyombo na kulea ila mtoto wa kiume yeye anatakiwa kusoma ilia je kuwa na
maisha mazuri hapo mbeleni.
Lakini pia
hata kwa upande wa kiuchumi pia ipo hivyo kwani mwanamke anatakiwa kukaa
nyumbani lakini baba ndio anatakiwa kutafuta pesa na hata mama akitafuta basi
inakuwa ni ya familia nzima siyo ya mama peke yake kama ilivyo kwa baba, na
hivyo hivyo hata katika masomo ilikuwa hivyo hapo nyuma kwa kuambiwa wewe mtoto
wa kike unatakiwa usome masomo rahisi kama ya arts na ukionekana unasoma masomo
ya sayansi unaambiwa unasoma masomo ya kiume.
Aliendelea kwa
kusema kuwa jambo lingine ni fikra mgando na hii ni kwa wale ambao wamejiwekea
kwamba huyu mwanamke basi kuna vitu hawezi kuvifanya kama kufanya biashara au
mwanamke kugombea uongozi anaonekana kama astahili wakati ni vitu ambavyo
anaweza kuvifanya, lakini pia kwa wanawake wenyewe kukubali kuwa kuna baadhi ya
kazi ni za wanaume hivyo wao hawawezi kama ukandalasi, urubani na vitu vingine vingi
hivyo ndio vinaitwa fikra mgando.
Aidha muwezeshaji
huyo alisisitiza swala la uwezeshaji wanawake na kusema kuwa ni vema
kuwawezesha wanawake na wasichana kuzitambua fursa chache walizo nazo katika
jamii yao na kuchukua hatua za haraka ili kubadilisha hali hiyo, na kuwapa
nguvu ya kushiriki katika maamuzi na hata kugombea nafasi mbalimbali za
uongozi.
Na mwisho
kabisa aliongelea bajeti yeye mlengo wa kijisia na kusema kuwa hii ni bajeti
shirikishi nan i yenye kulenga makundi yote katika ngazi zote za jamii bila
kumuacha hata mmoja nyuma ikiwa walemavu, wazee na watoto vijana wakina mama na
makundi yote yaweze kufikiwa na bajeti hii ili kuondoa tatizo la kuonekena
imeelemea upande mmoja.
No comments:
Post a Comment