Sunday, December 3, 2017

JIJI LA DAR ES SALAAM LAINGIA KATIKA MASHINDANO NA MIJI MIKUBWA DUNIANI KAMA NEW YORK CITY.

Jiji la Dar es salaam laingia katika mashindano ya miji inayokuwa kwa kasi zaidi duniani likishindanishwa na miji mikubwa kama New York, Cap Town, St. poul, Nairobi nk.
Tokeo la picha la dar es salaam
Hayo yamesemwa mapema jana na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam  Mh. Isaya Mwita alipokuwa akijiandaa na safari ya kuelekea katika jimbo la Chicago nchini marekani katika mkutano wa mameya zaidi ya 84 duniani kote.

Mkutano huo wenye lengo la kuwakutanisha mameya toka pande zote za dunia ili  kuwajengea uwezo wa jinsi ya kuziongoza Serikali za Mitaa(Local government) na namna ya kuongeza mapato katika Halmashauri zao.

Hata hivyo Meya Mwita alisema kuwa jiji la Dar es salaam ambalo linawakazi zaidi ya milioni sita na ni jiji la tatu barani afrika kwa kukua kwa kasi katika maendeleo, na hii ikiwa ni kutokana na kuwepo kwa huduma muhimu za kijamii kama afya, maji pamoja na miundo mbinu mizuri.
Meya huyo aliendelea kusema kuwa katika mashindano hayo yanayohusisha miundo mbinu jiji la Dar es salaam limeingiza mradi wa UDART ambao maarufu kama mwendo kasi ili kuweza kupambana na miji hiyo mikubwa duniani.

Katika safari hiyo Mh. Mwita aliwataka watanzania kuwa wamoja na kumuombea ili awakilishe vema jiji letu na hatimaye tuweze kuibuka washindi, Meya ameondoka jana tarehe 2 na ataweza kurudi nchini tarehe 7 ya mwezi novemba  2017.

                  

No comments: