Mkuu wa
wilaya ya Ilala Mh. Sofia Mjema amewataka wanasheria kuacha kukaa ofisini
kusubiri kesi na badala yake kuingia mitaani kuwapa msaada wa kisheria wananchi
ambao wanaonewa kwa kutofahamu sharia na haki zao.
Aliyasema hayo
mapema leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizindua maadhimisho ya wiki ya
msaada wa kisheria ambapo alimuwakilisha Waziri wa Katiba na Sharia Prof. Palamagamba
John Kabudi.
Maadhimisho hayo
yanafanyika katika kanda zote saba za Tanzania ikiwa Kanda ya kusini, Kanda ya
Kaskazini, Kanda ya Nyanda za juu kusini, Kanda ya Ziwa nk. Na kwa kanda ya
pwani yamefanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Akiongea kwa
niaba ya Waziri wa Katiba na Sharia Mh. Sofia Mjema alisema kuwa maadhimisho
hayo yameaza leo tarehe 4 mpaka nane mwezi huu wa 12 na washiriki wakiwa ni Mahakama
kuu, na mashirika binafsi yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria kama LSF, TLS, LHRC, TAMWA, WLAC, TAWLA nk.
Mkuu wa
wilaya huyo aliendelea kusema kuwa ni kwa mara ya kwanza maadhimisho hayo
yanafanyika chini ya wizara ya katiba na sharia na hapo mwanzo yalikuwa
yakiratibiwa na mashirika binafi.
Na kauli
mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “Msaada wa kisheria kwa maendeleo ya wananchi”
Baadhi ya wageni walioudhuria katika maadhimisho ya Wiki ya msaada wa kisheria yaliyofanyika mapema leo viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam |
Lakini pia
jitihada za mashirika hayo zimeweza kuzaa matunda kwa kukaa chini kwa pamoja na
wizara na kuunda sharia Namba 1 ya mwaka 2017 ambayo inaonyesha kutambulika kwa
huduma hii kwa serikali ambapo mwanzo ilikuwa haijatambuliwa rasmi.
Mh. Mjema
aliendelea kusema kuwa lengo kuu la maadhimisho hayo ni kujaribu kujenga
ukaribu kati ya wanasheria na wanachi pamoja na kuwarudishia elimu hii ikiwa ni
kama shukrani kwa wananchi hao kwa kuweza kuwapa msaada huo wa kisheria.
Na “Pia
inaeleweka kuwa wananchi wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu sharia lakini pia
hawana hata uwezo wa kulipia mawakili wa kuwasimamia katika kesi zao hivyo husababisha
kukosa haki zao au kuonewa, na kutokana na hili wanahitaji msaada wa kisheria ambao
utakuwa ni mkombozi wao”. Alisema Mjema
No comments:
Post a Comment