Thursday, December 14, 2017

QNET: Biashara ya ‘Masoko-Mtandao’ ni halisi, yenye maadili


Kama ambavyo mjadala unavyoendelea miongoni mwa wataalamu, wafanyabiashara, wataalamu wa masoko, vyombo vya habari na umma kwa ujumla kuhusu uhalali wa biashara ya mauzo ya moja kwa moja au mtindo wa masoko ya moja kwa moja kama biashara halali, yenye maadili. 

QNET TANZANIA, kampuni ya masoko ya moja kwa moja ambayo hivi karibuni imefungua wakala wake jijini Dar es salaam, wamejitumbukiza katika mada wakiweka wazi hoja kuhusu mtindo huu wa biashara na kuondoa wasiwasi wowote uliopo kwamba biashara ya mauzo ya moja kwa moja haizingatii taratibu za kibiashara za kimataifa. 

Katika mahojiano maalumu na vyombo vya habari, Mwakilishi wa QNET Tanzania hapa nchini, BENJAMIN MARIKI anajibu baadhi ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu mtindo wa biashara za mauzo ya moja kwa moja.
Nukuu kwa Ufupi:

Swali: Biashara ya moja kwa moja ni nini/ mtindo wa biashara ya masoko -mtandao ni nini?
Jibu: Biashara ya mauzo ya moja kwa moja inahusu mauzo ya bidhaa au huduma kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine mbali na maeneo ya maduka ya reja reja yalipo. Mfumo huu wa biashara ya mauzo ina zaidi ya umri wa miaka 100 ulimwenguni na mwanzoni kabisa ilianzaia katoka nchi ya Marekani. Leo, ni sekta ya biashara yenye thamani ya dola za kimarekani  bilioni 180 ulimwenguni kote ikiwa inajumuisha takribani watu milioni 180.

Jinsi gani watu wanaojihusisha na masoko ya mtandao wanavyojipatia kipato?
Watu wanaojihusisha na biashara za moja kwa moja au biashara za masoko-mtandao wanajipatia gawio kutokana na mauzo ya bidhaa au huduma ambayo hukokotolewa kwa mtindo wa fidia kutoka katika kampuni ambayo wanaiwakilisha. Mtindo wa biasbara ya moja kwa moja unatoa fursa kwa mtu binafsi kujipatia kipato kupitia kujiajiri mwenyewe na kufanya kazi kwa bidii. Masoko ya mtandao ni moja kati ya mifumo maarufu ya mauzo ya moja kwa moja.

Kuna tofauti gani kati ya Biashara ya Masoko-mtandao na ‘Mpango wa Upatu’ (Pyramid Scheme)?

Biashara ya Masoko-Mtandao sio mpango wa kujitajirisha haraka. Inaweza kuwa ni yenye faida kubwa, lakini pia ni biashara ngumu. Tangu mwanzoni, biashara halali itakuambia kwamba matokeo yatakuja pale tu utakapoweka juhudi na muda. Kampuni yoyote ambayo inakuahidi kuwa utapata utajiri kwa urahisi lazima itazamwe kwa tahadhari. Kwa mafano, QNET jna maelezo ya tahadhari kizuizi kuhusu kipato katika mtandao wake na nyaraka zake za masoko.

Kampuni za masoko ya mtandao yanatoa bidhaa zenye ubora au huduma tofauti na mpango wa upatu ambao huwa hauna bidhaa halali au huduma. Makampuni bora ya biashara za masoko ya mtandao hutumia kiasi kikubwa cha fedha kufanya utafiti na kutengeneza bidhaa bora ambazo zinatumiwa na watu wakati upatu hauna utaratibu huo.
QNET, Kwa mfano, inatoa zaidi ya bidhaa 300 tofauti katika makundi 9 ya bidhaa tofauti tofauti.
Zaidi ya hapo, biashara ya masoko ya mtandao huwa yana ukomo katika mpango wa ukomo wao ambayo huwa inadhibiti idadi ya watu ambao wanaweza kujipatia gawio kupitia mauzo. Hii inakusudia kusawazisha uwiano miongoni mwa washiriki. Katika mfumo wa ‘piramidi’ watu walioko mstari wa juu au wale ambao ‘wako juu’ hupata fedha nyingi wakati wale walioko mstari wa chini au wale ‘walioko chini’ mara nyingi huwa wanaachwa nyuma kutokana na kujiunga kwa kuchelewa.
Katika kampuni ya QNET, kila mtu anaweza kufanikiwa bila kujali alianza lini na mafanikio ya mwakilishi wa kujitegemea (IR) ambaye anasambaza bidhaa hutegemea na mafanikio ya watu walioko katika timu yake.
Kwa kuongezea, Makampuni halali ya biashara za masoko ya mtandao huwa ya na mfumo imara wa mafunzo ambao huwa unaweka msisitizo katika mafunzo kwa wauzaji katika mtandao wao. Makampuni ambayo yanajali wasambazaji wao kwa dhati na wanataka wafanikiwe ndio ambao wanatoa zana za kibiashara na mafunzo kuwasaidia kukuza biashara zao. Makampuni kama vile QNET yana wakufunzi wenye sifa wenye utaalamu na uzoefu kwaajili ya kuwasaidia wanachama wao waweze kuelewa vyema biashara na bidhaa na kufanya kazi kama washauri na wahamasishaji kwaajili ya kukuza biashara.
Kwa kumalizia, makampuni ya biashara ya masoko ya mtandao yana sera na taratibu nzuri pamoja na kanuni za maadili. Kampuni yoyote halali ya biashara ya mtandao huwa ina lengo la kufikia ukuaji endelevu kwa kudumisha utamadunj wa mauzo yenye maadili. QNET inaweka msisistizo mkubwa sana katika kanuni za maadili ya utendaji kwa wawakilishi wake na kuwapatia miongozo ya kina kuhusu ufanyaji wa biashara ya masoko ya mtandao kitaalamu  pamoja na sera na taratjbu zake.
Masoko ya mtandao yanajivunia kukuza na kuendeleza wajasiriamali; jinsi gani inawawezesha wajasiriamali wa ndani katika kuendeleza biashara zao?
QNET Inatoa msisitizo mkubwa sana katika mafunzo na elimu kwa wawakilishi binafsi (IRs). Hatuweki mkazo katika kuendeleza uwezo wao wa kitaalamu tu bali pia tunatilia mkazo katika ukuaji binafsi na maendeleo. Tunaamini kwamba mafanikio ya kifedha peke yake hayatoshelezi. Tunanaamini kwamba tunahitaji kuwaendeleza watu kuwa wanadamu bora ili waweze kutumia mafanikio yao kuchangia maendeleo ya jamii zao.
QNET inashirikiana na makampuni bora ya mafunzo na biashara za masoko ya mtandao ambayo yamefanikiwa katika kutoa mafunzo kwa wakufunzi ambayo wanahamasisha wakufunzi kutoa elimu hii kwa watu wengine zaidi katika timu zao kwa lugha zao wenyewe. Wakati mafunzo ya biashara unazingatia mpango wa ulipaji wa fidia, kutokana na uuzaji wa bidhaa na cha muhimu zaidi, umuhimu wa maadili na ufanyaji wa mauzo kwa kitaalamu, ni programu ya mafunzo ambayo sio ya kibiashara ambayo ndio maarufu zaidi na yenye athari zaidi.

Mada zinazofundishwa katika mafunzo ya maendeleo binafsi yanajumuisha kupokea mabadiliko, kukabikiana na changamoto na kukataliwa, kujenga na kuendeleza mahusiano, mawasiliano yenye tija na pia muonekano binafsi.

Programu za mafunzo zinatofautiana kutoka katika kundi dogo la washiriki 20-30 mpaka washiriki 1000 kwa mafunzo ya kanda. Mafunzo ya ulimwengu huenda kwa maelfu ya washiriki na hufanyika kwa siku kadhaa.

Mifano michache ya programu za mafunzo na uzoefu ambayo IR anaweza kunufaika nazo ni:

Mfululizo wa semina za kutengeneza mtandao (NSS) – NSS inatoa mafunzo ya kujenga mtandao na kuhamasisha ambayo husaidia kuboresha mikakati na mbinu na kusaidia katika maendeleo binafsi na ya kitaalamu ya IR. Tukio hili huwa linaandaliwa mahsusi kwaajili ya kutatua mahitaji maahususi ya mtandao katika nchi au jiji fulani.

Semina ya Mambo ya Biashara ya Mtandao (NBS) Haya ni mafunzo ambayo huhudhuriwa na washiriki wachache kuliko NSS lakini huwa yana moduli zile zile, mwelekeo na malengo yale yale.  

Mafunzo ya Bidhaa – Huwa ni programu ya mafunzo ya kina ambayo hufundisha IR kuhusu mambo yote ya msingi kuhusu bidhaa zinazouzwa chini ya bango la QNET. Mafunzo yanaweza kufanyika katika makundi madogo madogo au kama mafunzo ya siku nzima ikihudhuriwa na watu wengi.

Mafunzo katika Mtandao – QNET hendesha mfululizo wa mafunzo katika mtandao (online) ambayo IRs anaweza kuhudhuria wakiwa nyumbani kwao kwa kuingia kupitia katika computer zao. Kuna kuwa na vipindi vya mazungumzo kuhusiana na mada mahususi  kama vile bidhaa mpya inayozinduliwa, sera na taratibu na mpango wa kufidiwa hufanyika katika lugha mbali mbali na viongozi wa mafunzo wa QNET.

Kongamano – QNET huandaa kongamano la mwaka la kimataifa kila mwaka huko Asia na Mashariki ya Kati kwa kipindi cha siku tano. Katika kongamano hilo takribani IR 8,000-10,000kutoka katoka zaidi ya nchi 40 hukutana pamoja kusikiliza  na kujifunza kutoka kwa wataalamu wa mafunzo na IR wengine waliofanikiwa kutoka duniani kote. Katika kongamano hili QNET pia huwa inaandaa maonyesho ya bidhaa ambayo huwaruhusu IR kushika na kufurahia bidhaa zetu, kuuliza maswali wataalamu na kuangalia mifano. Kongamano huwa pia linafanyika katika kiwango kidogo kulenga kanda fulani mahususi katika kipindi chote cha mwaka.

Zaidi ya Tanzania, ni wapi ambako QNET ina ofisi zake ndani ya Afrika?
Tumetengeneza msingi mzuri wa kibiashara katika nchi za Ivory Coast, Burkina Faso, Cameroon, Mali, Guinea and Senegali.
Ni aina gani ya bidhaa na huduma ambazo mnazo wakati wote?
Kupitia usimamizi imara wa ubora na kufanya kazi na watafiti wa kiwango cha juu, wanasayansi na wazalishaji katika kila idara, QNET inatoa aina mbalimbali za bidhaa za mitindo ya kimaisha na afya ambazo zimethibitisha ufanisi wake kwa watu duniani kote. Kutoka katika huduma binafsi, lishe, vipodozi, bidhaa za utunzaji wa nyumba na mwili, nguvu za maji, mpaka katika mapambo ya vito na saa za mkononi, na vifurushi vya sikukuu.

Ni kiasi gani cha mtaji ambacho mjasiriamali anayeanza anahitaji kuwa nacho kuweza kuanzisha biashara hii?
Mjasiriamali anahitaji Dola 30 (TZS 66,000) kujiandikisha kwaajili ya kuanza biashara hii.

Biashara za masoko yamtandao kwa ujumla inachukuliwa vibaya na baadhi ya watu katika jamii, lini kwa mtazamo wa QNET, biashara hii inaweza kuanza kuchukuliwa kwa mwonekano mzuri (chanya)?
Kwa utandawazi na kuondolewa kwa vizuizi vya biashara, ni suala la muda tu kabla ya sekta hii kuanza kupewa mtazamo mzuri zaidi.

No comments: