Saturday, December 30, 2017

TRA WAJA NA HILI KWA ASKOFU KAKOBE

Kufuatia Kauli ya Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakary Kakobe kudai kuwa ana pesa nyingi kuliko serikali, mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamepanga kumchunguza kiongozi huyo wa dini.
Tokeo la picha la ASKOFU KAKOBEHayo yamesemwa leo na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo amesema;

“Tupokea kauli ya Askofu Kakobe kwa unyenyekevu mkubwa sana kwa kuwa wao wanapenda watu wenye pesa nyingi ili waweze kupata haki yao

“Kama mtu ana hela kuliko serikali, kama ambavyo tunajua serikali yetu inatoa huduma inanunua ndege, imejenga standard gauge, inajenga barabara, inatoa elimu bure, inalipa mishahara kwa watumishi wa umma, inalipia madawa hospitalini, inalipa na kutoa huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi. Lakini Serikali hiyo tunaambiwa inazidiwa hela na Askofu Kakobe basi ni jambo jema.

“Tunawafahamu matajiri wanalipa kodi, baada ya kauli ya Askofu Kakobe tukaanza kupitia kumbukumbu zetu ili kuona namna Askofu Kakobe anavyolipa Kodi. Kakobe aliyesema anaizidi Serikali kwa pesa hakuna kumbukumbu za ulipaji kodi wake. Sisi Wataalamu wa mambo ya kodi tutafahamu tu kama utajiri wake anaousema unatokana na sadaka tu au kuna shughuli nyingine za kiuchumi anafanya”

“Tunaelewa kwa mujibu wa sheria sadaka haitozwi kodi, ila tunafahamu taasisi za dini huwa zina shughuli nyingine za kiuchumi, huenda Askofu Kakobe na yeye akawa na shughuli nyingine zinampatia hela mpaka akawa na pesa nyingi kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini pia kama kweli ni sadaka pekee inayomfanya Askofu Kakobe awe na pesa nyingi kuliko Serikali ni jambo la kushtua kidogo. Basi hizo sadaka ni nyingi kweli kweli na watoa sadaka watakuwa matajiri kweli kweli,” alisema Kichere.

Aidha TRA wamemtaka Askofu Kakobe kutoa ushirikiano ili wajiridhishe juu ya utajiri wake na ulipaji kodi wake.

No comments: