Saturday, December 9, 2017

UMOJA WA MATAIFA HIVI NDIVYO ULIVYOLICHUKULIA TUKIO LA KUFA KWA WANAJESHI WA TANZANIA NCHINI CONGO

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio lililotekelezwa katika kambi ya walinzi wa amani iliyopo Semuliki, Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kupelekea vifo vya wanajeshi 20 huku wengine 53 wakijeruhiwa.
Image result for wanajeshi wa tanzania waliokufa congo
Kambi ya jeshi hilo la ulinzi wa amani (MONUSCO) ilishambuliwa Disemba 7 jioni na kupelekea vifo vya wanajeshi 15 wa Tanzania na 5 wa DRC.

Wajumbe hao wametuma salamu za pole kwa familia za wafiwa, serikali ya Tanzania na DRC lakini pia MONUSCO huku wakiwatakia majeruhi afya njema na wapone haraka.

Aidha, katika taarifa hiyo wajumbe hao wameeleza kuwa kushambulia kambi za walinzi wa amani ni tukio ambalo linachukuliwa kuwa ni uhalifu wa kivita katika sheria za kimataifa na kwamba wahusika hawawezi kusamehewa kwa matendo hayo.

Serikali ya DRC imetakiwa kuhakikisha kuwa wahusika wa tukio hilo wanakamtwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria na kutaka makundi yote ya kihalifu kusitisha mapigano.

Pia, wamewashukuru wanajeshi na watu mbalimbali ambao wanahatarisha maisha yao kila siku kwa ajili ya kuhakikisha amani inakuwepo duniani, na kwamba tukio kama hilo la kusikitisha linaikumbusha dunia kuwa ni kiasi gani watu hawa wameweka maisha yao hatarini kwa faida ya wengi.

Shambulio hilo la DRC ni kubwa zaidi kuwakumba walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa kwa miaka ya hivi karibuni.

Baraza la Usalama alimesema kwamba litaendelea kushirikiana kwa karibu na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN nchini DRC na MONUSCO kuhakikisha kuwa wanatekeleza ipasavyo malengo yao.

No comments: