Upungufu wa
matundu ya vyoo katika shule za msingi limeendelea kuwa ni tatizo kubwa katika
shule mbalimbali za jiji la Dar es salaam.
Imebainika
kuwa shule nyingi hasa za msingi idadi ya matundu haiendani na idadi ya wanafunzi
katika shule zilizopo Dar es salaam hata mikoani pia.
Hayo
yamesemwa mapema wiki hii na wanaharakati wa GDSS walipokuwa wanawasilisha
ripoti ya zoezi walilopewa la kwenda kuulizia vipaumbele vilivyohainishwa
katika serikali zao za mitaa kwa ajili ya bajeti kuu ya taifa ya mwaka 2017/18.
Katika zoezi
hilo zilipata nafasi kata tatu kuweza kuwasilisha vipambele vyao walivyoweka
katika kata zao, na kata hizo ni Kipunguni, Makumbusho na kata ya Mabibo.
Muwakilishi wa Kata ya Kipunguni Ndugu. Selemani Bishagazi akiwasilisha vipaumbele walivyoviweka katika kata yao ya Kipunguni mapema wiki katika semina ya GDSS. |
Kata ya
Kipunguni na Makumbusho zimeonekana kuwa na matatizo yanayofanana kwa kuwa
katika vipaumbele vyao wote walidai kuongezewa matundu ya vyoo katika shule zao
pamoja na Zahanati ndio vitu wenye uhitaji navyo mkubwa katika maeneo yao.
Na Kipunguni
ni kata mpya hivyo bado serikali haikuweka zahanati katika kata hiyo, na kata
ya Makumbusho mwanzo walikuwa wakitumia hospitali ya Mwananyamara ambayo kwa
sasa imekuwa Hospitali ya Rufaa na inakataa kupokea wagonjwa wa kawaida na
kuwataka wapewe rufaa ndipo waende hospitalini hapo.
Kwa upande
wa Kipunguni wao pia waliomba Kituo cha Polisi kwa kuwa katika eneo lao hakuna
kituo hiyvo inawalazimu kutumia vituo vilivyopo kata nyingine kama Gongo la
mboto nk, lakini pia waliomba vitambaa vya kujiifadhia watoto wakike(Pad) wawapo
katika siku zao.
Licha ya
kudai matundu ya vyoo na Zahanati Makumbusho kipaumbele chao kingine kilikuwa
ni ukarabati wa shule ya Mwananyamara na Mianzini kwani mvua ikinyesha inaingia
darasani na kufanya watoto kushindwa kusoma mpka wasubiri mvua ziishe.
Lakini pia
wakazi wa Makumbusho waliomba kuwekewa ukuta katika shule zao kwani uvamizi wa
watu unazidi mpaka katika maeneo ya shule na kufanya wanafunzi kushindwa kusoma
akili na mawazo yao yanakuwa nje darasa.
Aidha katika
hizi kata zote kata ya Mabibo imeonekana kuwa na changamoto chache sana na
nyingi zikiwa tayari zimeshapatiwa ufumbuzi wake, ikiwa waliomba million 15 kwa
ajili ya kujenga jingo jipya na ukuta ukuta wa Zahanati ya Mabibo vyote
vimeweza kufanikishwa.
Wanaharakati kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaa wakimsikiliza kwa makini muwasilishaji wa vipumbele vya kata ya Mabibo ndugu. Msafiri Shabani Mapema wiki hii jijini Dar es salaam. |
Na jambo lingine
lilikuwa ni vyumba vya kujiifadhia watoto wa kike na wakiume Mwalimu Mkuu wa Jeshini
ameahidi kutoa vyumba viwili na Mwalimu wa Umoja ametoa ahadi ya kutoa kimoja,
lakini pia walikuwa na mradi wa kujega shule ya Sekondari Kawawa wameshapata
mfadhili na ujenzi utaanza hivi karibuni.
Na mwisho
kabisa walikuwa na changamoto ya ujenzi wa Kivuko cha TASAF kilichoalibika na
mvua, walineda kuwaomba msaada kiwanda cha NIDA Textile
wameambiwa watapewa million
20 kwa ujenzi huo na million 5 zilizobaki waombe Halmashauri.
Ndugu. Innocent Sirriwo akitoa maoni yake kuhusu mawasilisho ya vipaumbele yalikuwa yakifanywa na wanaharakati mbalimbali wa jiji la Dar es salaam. |
No comments:
Post a Comment