Sunday, January 21, 2018

ACT WAZALENDO WAGOMEA UCHAGUZI WA MARUDIO WA JIMBO LA SIHA NA KINONDONI SOMA HAPA SABABU ZA KUGOMA HUKO...

Chama cha ACT Wazalendo, kimesema hakitashiriki kwenye uchaguzi wa ubunge kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha kutokana na kutoridhishwa na hali halisi na mazingira yaliyoandaliwa na tume ya uchaguzi (NEC).
Tokeo la picha la act wazalendo
ACT kimesema kwamba chama tawala kinatumia jeshi la polisi na watendaji wa serikali, ili kutengeneza mazingira ya kuwatisha wananchi na kuiba kura hata pale inapotokea wapinzani wameshinda. Hayo yamesemwa leo na chama hicho kilipokutana na waandishi wa habari ambapo Msafiri Mtamelwa, Ado Shaibu na Idrisa Koeta ndiyo waliokuwa wazungumzaji wakuu.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho-Bara, Msafiri Mtemelwa amesema changamoto walizozilalamikia katika uchaguzi wa Januari 13 katika majimbo ya Singida Kaskazini, Songea Mjini na Longido bado hazijafanyiwa kazi.

Amesema malalamiko ya chama hicho kwa NEC ni matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola dhidi ya vyama vya upinzani kwa lengo la kukisaidia chama tawala CCM.

Uchaguzi wa Siha na Kinondoni unafanyika baada ya waliokuwa wabunge wa majimbo hayo kuhamia CCM Desemba mwaka jana.

No comments: