Wednesday, January 24, 2018

VITENDO VYA UKATILI WA WATOTO VIMEENDELEA KUONGEZEKA ENEO LA CHASIMBA BUNJU JIJINI DAR ES ALAAM

Picha ni Prepetua Martine ambae ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wa Basihaya.
Khadija Mahamba Dar es salaam.

Licha ya serikali na wanaharakati mbalimbali kupinga vikali unyanyasaji wa watoto lakini bado tatizo hili linaonekana kutokoma katika baadhi ya maeneo ikiwemo Chasimba bunju jijini Dar es salaam

Akiongea na habari 24 Bi. Prepetua Martine ambae ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wa Basihaya na makamu mwenyekiti wa  jukwaa hilo kwa kata ya Bunju amesema unyanyasaji wa watoto na malezi mabovu ya kulala chumba kimoja wazazi na watoto wao  kwa baadhi ya wazaza wa mtaa wa Chasimba yamekuwa ni changamoto kubwa katika mtaa huo.

Aidha ameongeza kuwa  ni vyema kila mtu  akawa mlinzi wa mwenzake dhidi ya matendo maovu yatayofanywa na jirani yake  ili kunusuru tatizo hilo ambalo limeshika kasi katika mtaa huo.
Mazingira halisi ya wakazi wa eneo la Chasimba Bunju jijini Dar es salaam.
Pia ametoa wito  kwa wananchi wa mtaa huo kutokaa kimya pindi waonapo matatizo ya unyanyasaji au tukio lolote ambalo ni uvunjifu wa sheria kwani kwa kukaa kimya kwao kutafanya watu kutobadilika na kuendeleza unyanyasaji.

Pia amewataka wazazi kuhakikisha  kila mtoto apelekwe Shule kwa mujibu wa sheria za nchi na kwa kipindi hiki ambacho mh. rais magufuli amejitolea kufanya elimu iwe bure.   

No comments: