Baadhi ya wakuu wa idara pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wakati alipokuwa akizungumza na kuelezea mikakati iliyopo mkoani humo. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwashukuru wananchi ambao wamekuwa wakijitoa kuunga juhudi za serikali za kuhakikisha kila eneo linatatuliwa changamoto zake. |
Na,Joel Maduka,Geita
Serikali
mkoani Geita imetangaza oparesheni ya
kuwafuatilia wazazi na walezi ambao watoto wao walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na kwamba hadi
sasa bado awajawapelekwa shuleni na
pindi watakapobainika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria .
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari amesema kuwa kwa sekondari hali sio nzuri ya wanafunzi ambao wametakiwa
kuingia kidato cha kwanza kwani hadi sasa asilimia 46 ya wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza hawajaripoti shuleni.
Luhumbi
ameongezea kwamba suala la elimu ni haki
ya mtoto na hayupo tayari kuona wazazi wanawaozesha ama kuwaajiri
kwenye shughuli za migodi na biashara ndogondogo watoto ambao wanaumri wa
kwenda shule na wamefaulu mtihani wa darasa la saba.
Ameendelea
kusema anafuatilia taarifa ya walimu
ambao wameonekana kuwa ni kikwaza kwa kuchangisha fedha na kwamba endapo
wakibaini hatua kali zitachukuliwa na kwamba amesikia kuna baadhi ya shule
walimu wameendelea kuwatoza fedha wanafunzi kinyume na sheria.
katika
mtihani wa darasa la saba mwaka jana wanafunzi 32,110 walifaulu na kuchaguliwa
kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu lakini hadi kufikia tarehe 18 janaury mwaka huu wameripoti wanafunzi 17,202 sawa na
asilimia 54 .
Kwa mujibu
wa Takwimu zilizotolewa na idara ya elimu mkoa inaonyesha wilaya ya Bukombe
walichaguliwa wanafunzi 3,985 na hadi sasa wameripoti 1,620 sawa na asilimia
41,Chato walichaguliwa 6,449 walioripoti ni 3,691 sawa na asilimia 57,Geita mji
walichaguliwa 4,286 walioripoti ni
2,751,sawa na asilimia 64 huku Mbogwe waliochaguliwa ni 3,029 walioripoti ni
1,924 sawa na asilimia 64.
Halmashauri
ya Geita vijijini wanafunzi 11,760 walichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza
lakini hadi sasa wameripoti wanafunzi 5,872 ambayo ni sawa na asilimia
50,wilaya ya Nyanghwale 2,601
walioripoti ni 1,344 sawa na asilimia 52
No comments:
Post a Comment