Wednesday, January 31, 2018

SOMA HAPA SERA ZA MTULIA AKIWAOMBA WANA KINONDONI WAMPE RIDHAA YA KUONGOZA TENA JIMBO HILO.


Image may contain: one or more people, people on stage, crowd and outdoor

Mgombea Ubunge katika jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CCM Maulid Said Mtulia akinadi sera zake jukwaani na kuomba kura kwa wapiga kura wa Kata ya Ndugumbi.


**********

*YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA KINONDONI, MAULID SAID MTULIA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI KATA YA NDUGUMBI JUMANNE JANUARI 30, 2018*

"Kama Mtulia angekuwa amenunuliwa asingepewa tena dhamana ya kugombea Ubunge " - Mtulia

"Ningekaaje kwenye chama ambacho Mwenyekiti na Katibu hawaelewani, nimejitoa ili niwe na uhuru wa kuwatumikia wana Kinondoni." - Mtulia


"Kile chama hamkusikia kimesimamisha wabunge 8, mlitaka nami nisimamishwe?" - Mtulia



"Mtulia nimejiuzulu ili kuwaokoa Wananchi wa jimbo la Kinondoni" - Mtulia


"Kuhama chama ili kujiunga na chama chenye maendeleo, huo ni usaliti?" - Mtulia

"Mtulia huyu ndio aliotoa hela yake mfukoni kujenga visima vya maji; Mtulia aliyefungua kesi mahakamani kuzuia bomoa bomoa; ndio Mtulia yule aliyeomba maghorofa ya Magomeni Watu waliojitokeza nyumba zao wakae bure" - Mtulia

"Mtulia mimi ni yule yule mkinichagua nitahakikisha naendelea kuwaletea maendeleo nikishirikiana na viongozi wenzangu na Rais wangu mpendwa Di. Magufuli " - Mtulia

"Ninaomba tena ridhaa ili nihakikishe nawaletea maendeleo wana Kinondoni kutokana na kugombea kwenye chama chenye ilani ya uchaguzi iliyoshikan dola" - Mtulia

"Naomba dhamana ya kugombea ili nikashirikiane na wenzangu kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 - 2020" - Mtulia

"Kazi yangu mkinichagua ni kwenda kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na si porojo wala usanii" - Mtulia

"Ukichagua Mtulia umechagua maendeleo; ukimchagua Mtulia umejenga daraja kati ya Wananchi na Serikali" - Mtulia

No comments: