Na Woinde Shizza,Kondoa
Wananchi wa vijiji 11 kwenye kata sita wilayani Kondoa wameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kumaliza migogoro inayotokea kati yao na Askari wa Pori la Akiba la mkungunero kwani wananchi hao wamekuwa wakibambikiwa kesi za mara kwa mara na Askari hao na kugeuzwa miradi kwa madai ya mifugo.
Wananchi wa vijiji 11 kwenye kata sita wilayani Kondoa wameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kumaliza migogoro inayotokea kati yao na Askari wa Pori la Akiba la mkungunero kwani wananchi hao wamekuwa wakibambikiwa kesi za mara kwa mara na Askari hao na kugeuzwa miradi kwa madai ya mifugo.
Licha
ya mda mrefu kupita na kutulia kwa migogoro pembezoni mwa pori la akiba
la Mkungunero na Wananchi wa vijiji 11 bado kumekuwa na kamata kamata
ya wananchi na kujikuta wanafunguliwa kesi ambapo mifugo zaidi ya 146
inashikiliwa na Askari wa wanyapori ndani ya hifadhi hiyo huku wananchi
watatu wakishikiliwa tokea demember 26 mwaka jana na kesi yao ipo mahakamani hadi december 5 mwezi huu.
Wakizungumza kwa niaba ya Wananchi hao Diwani wa Kata ya
Itaswi Issa Chobu alisema kuwa licha ya mgororo huo kuwepo kwa mda mrefu lakini
Tatizo kubwa ni Serikali kushindwa kufuatilia ripoti ya tume iliyoundwa waziri
mkuu ya mwaka 2012 ili wananchi waliohamishwa ndani ya hifadhi wakati huo
walipwe fidia zao.
Alisema kuwa licha ya wananchi kukaa na viongozi wa Pori
hilo la Akiba na kuona wanatatatuaje matatizo ya unyweshaji wa maji mifugo na
wananchi kutumia maji hayo kwa matumizi yao bado tatizo kubwa kwenye mgogoro
huo ni huduma bora ya maji na hilo litaondoa tatizo la mifugo na wananchi
kuingia ndani ya hifadhi .
“Mimi kama mwakilishi wa wananchi naiomba serikali kuangalia
upya ripoti ya tume iliyoundwa na waziri mkuu pinda wakati huo naona hii
itasaidia kuondoa dhana nzima ya migogoro na kurudisha uhifadhi shirikishi kwa
maendeleo ya taifa na uhifadhi.”alisema Chobu
Nae Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kutish Adamu Ally amesema
kuwa wao kama majirani wema wa hifadhi waliomba kunywesha mifugo kwenye mto
unaoanzia milima ya haubi na kupita mita 120 ndani ya hifadhi karibu na
kitongoji changu katika kikao chao na viongozi wa pori hilo la Akiba mwezi wa
Tano mwaka jana na kukubaliwa lakini kwa kipindi cha kiangazi lakini cha
kushangaza kila wakipeleka mifugo kunyesha wamekuwa wakikamatwa na kutozwa
kiasi cha 50,000 kwa kichwa cha mfugo.
Alisema kuwa wamekuwa wakitoa malalamiko yao mara kwa mara
lakini wananchi wameendelea kukamatwa na kufunguliwa kesi kama wenzao watatu
wamekamatwa toka desember 26 na kufikishwa mahakamani licha ya wao kutokuwepo wakati
mifugo inakamatwa.
Juhudi za kumpata Meneja wa Pori hilo la Akiba kwa njia ya
Simu zinaendelea licha ya kuwa alikuwa hapatikani hewani ili aweze kujibu
tuhuma hizo zilizoelekezwa kwenye uongozi na watumishi wa Poti hilo la Akiba la
Mkungunero
Gazeti hili limefika kwenye eneo la tukio na kujionea na
kusikiliza pande mbali mbali za serikali za vijiji hiyo na kata na kugundua
kama serikali itafuata ushauri huu basi mgogoro huo utakuwa Historia,Moja
Kuanzisha(WMA) Uhifadhi shirikishi,Pili uwepo wa Ujirani Mwema,na Tatu kuisaidia huduma za kijamii kwa mapato
inayotokana na uwindaji kwenye hifadhi hizo za Akiba.
No comments:
Post a Comment