Saturday, January 27, 2018

YALIYOTOKEA KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA KINONDONI KWA UPANDE WA CHADEMA,

LEO ikiwa ni siku ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa marudio wa jimbo Siha pamoja na Kinondoni, viongozi mbalimbali wa Chadema wamejaribu kumuombea ridhaa ya kupigiwa kura na wananchi, Katibu Mkuu wa chama hicho kwa upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu anayewania ubunge wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Saidi Kubenea:
"Nina mfahamu Salum Mwalimu ni kati ya waandishi wa habari wachache nchi hii walio jasiri na wasioogopa wanafanya kile wanachokiamini, ameandika stori kubwa na kuripoti matokeo makubwa sana na kutetea hadhi za binadamu, amefanya kazi kubwa kutetea misingi ya uandishi wa habari mkimpeleka Bungeni mtakuwa mmetupeleka chachu nyingine, mtakua mmemleta Lissu mwingine mdogo na kwenda kumpandikiza Bungeni" alisema Kubenea

Mbali na hilo Kubenea aliwataka wananchi kupuuza maneno yanasosambazwa kuwa Salum Mwalimu si Mtanzania na kusema huyo ni raia wa Tanzania na amekulia Tanzania bara hivyo waachane na maneno hayo yanayosambazwa na watu wa Chama Cha Mapinduzi.

Prof Jay: 
“Uwezo na sera za Mtulia tunazijua, nawza kutumia maneno makali lakini huo ndiyo ukweli, amewadharau sana watu wa Kinondoni. Tanazania nzima itatushangaa na tutakuwa tumeidharirisha Demokrasia, bora kuzungumza mengine kuliko habari za Mtulia.”

Sumaye;
“Kama wewe ni mbunge halafu umehama chama, basi haufai. Hizo pesa za kurudia uchaguzi zingeweza kuleta miundombinu ikwa wananchi. Katiba inaruhusu kutoa maoni lekini leo ukitoa maoni yako unaambiwa mchohcezi. Vikao vya bunge hatuvioni kwenye Televisheni. Je, hii katiba ilibadilishwa ili kuzuia bunge lisionyeshwe?”

No comments: