Monday, February 5, 2018

POLISI WAPEWA MAFUNZO YA USHAURI NASIHI KWA MUDA WA SIKU TANO NA JUKWAA LA UTU WA MTOTO(CDF)

Baadhi ya askari polisi waliopata nafasi ya kuhudhuria semina ya mafunzo ya ushauri nasihi kwa polisi wa dawati la jinsia wametakiwa kuitumia elimu hiyo vizuri kwa maslahi ya wananchi, lakini pia kuitumia elimu hiyo katika maisha yao ya kila siku ili iweze kuleta tija na manufaa kwao.

Kamishna wa Jeshi la Polisi kitengo cha polisi jamii Mussa Ally Mussa akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema leo katika ufunguzi wa semina ya siku tano ya kuwajengea uwezo polisi wa dawati la jinsia.
Hayo yamesemwa mapema leo na Kamishna wa Jeshi la Polisi kitengo cha polisi jamii Mussa Ally Mussa alipokuwa akifungua mafunzo ya siku 5 kwa polisi wa dawati la jinsia yaliyowakutanisha askari zaidi ya 50 mapema leo katika chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini jijini Dar es salaam.

Kamishna Mussa amesema licha ya wananchi kujitokeza kwenye madawati ya Kijinsia kwenye vituo vya Polisi na kusaidiwa matatizo yanayowakabili lakini bado wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la ukosefu wa ushauri wa nasihi.

"Mmekuwa mnawasaidia sana wananchi wanapokuja kwenye madawati, lakini licha ya kuwaidia bado kichwani mwao wanakuwa na tatizo la ukosefu wa elimu  nasihi ambayo inaweza kusababisha hata kuwa na katili huko mbeleni"
meza kuu wakisikiza utaratibu unaotolewa na mshereheshaji.
"Na ndio maana tunaomba sana mna hakikisha mnajaribu kutoa elimu ili waweze kuondokana na tatizo hili la kutopata  wa Ushauri nasihi"Amesema Kamishna Mussa.

Hata Hivyo,Kamishna Mussa amewataka Maafisa hao wa Polisi kuipa uzito semina hiyo ili waweze kupata kile kinachokusudiwa cha kuisadia jamii .

"Lengo langu nafahamu mtapata kile kinachokusudia katika semina hii,maana mmekuwa na changamoto katika utendaji wa kazi ,naimani semina hii itawasaidia katika kuondokana na Changamoto mbali mbali katika sehemu za kazi."ameongeza kusema.

Na mwisho kamishna hiyo alipenda kuwashukuru Jukwaa la Utu wa Mtoto kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden kwa kuweza kuona kuna umuhimu wa kuwapatia polisi wetu mafunzo ya ushauri nasihi ili waweze kufanya vema katika maeneo yao ya kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF akitoa ufafanuzi wa namna shirika hilo linavyoshirikiana na jeshi la polisi katika kuhakikisha haki za watoto zinapatikana, mapema leo Kurasini jijini Dar es salaam.
kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Bw. Koshuma Mtengeti amesema kuwa anawashukuru sana polisi kwani mara kwa mara wamejaribu kuwapa ushirikiano mzuri katika kufanikisha kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto.

"Lakini pia tunaendelea kufanya kazi kwa pamoja na jeshi la polisi hii ikiwa ni kuendelea kuboresha huduma katika dawati la jinsia na mambo mengine mengi, kama mwaka jana tumezindua mfumo wa kukusanya na kutoa taarifa za matukio mbalimbali ya ukatili wa kijinsia" alisema mkurugenzi

aliendelea kusema kuwa dawati la jinsia limeendelea kufanya kazi nzuri na hii ni kutokana na semina walizojaribu kuwapatia na wataendelea kufanya hivyo kwa kuhakikisha semina hizo zinakuwa endelevu ili maafisa wa polisi kitengo cha dawati la jinsia kuendelea kutoa huduma stahiki kwa jamii.
Baadhi ya Askari polisi wakifuatilia kwa umakini zoezi la ufunguzi wa semina hiyo ya siku tano iliyofadhiliwa na Jukwaa la Utu wa Mtoto, mapema leo jijini Dar es alaam.
Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa CDF itaendelea kutoa mafunzo hayo kwa makamanda wa mikoa mbalimbali ya hapa nchini wa kitengo cha dawati la jinsia ili kuendelea kuboresha huduma hiyo na kwa mwaka huu wataanza na mikoa kama Dar es salaam, Dodoma na Mara.

No comments: