NA VICENT MACHA - DAR ES SALAAM
Vijana
wametakiwa kuwa na moyo wa kujituma na
kuacha tabia ya kusubiri kuajiliwa na matokeo yake kuweza kujiajiri kwa kazi za
mikono na ujasiriamali.
Hayo
yamesemwa mapema jana na Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Huria cha Dar es salaam Profesa
Elifa Bisanda alipokuwa akisaini mkataba kati ya chuo hicho na shirika la Korea
kuhusu mafunzo ya elimu ya moyo chuoni hapo.
Akiongea na
waandishi wa habari Makamu ya chuo hicho alisema kuwa lengo la shirika hilo la
IYF ni kusambaza huduma hii duniani kote ya kuweza kuwa na elimu ya kujitegemea
ambayo hapa nchini kwetu iliasisiwa na marehemu Baba wa Taifa.
Aliendelea
kusema kuwa faida ya elimu hii kwa vijana ni kuweza kujiongoza wenyewe katika
kujitafutia maisha ili wasiwe tegemezi kwa wazazi na kwa kutoa lawama kwa
serikali kuwa hakuna ajira.
Aidha prof.
basinda alisema kuwa elimu hii imesaidia nchi nyingi kama Korea Kusini yenyewe
kwa kuwa na uchumi mzuri bila kutegemea rasirimali zozote za taifa na kumefanya
sasa kuwa ni nchi yenye uchumi mkubwa duniani.
“Lakini pia kusaini
mkataba huu aimaanishi ni kwa chuo kikuu huria peke yake bali hii nafasi
imetolewa kwa wanafunzi wa vyuo vyote hapa nchini lakini kitovu kimekuwa ni
hapa chuoni kwetu” alisema Profesa Basinda
“Na pia
jambo lingine zuri ni kwamba IYF itakusanya vijana kutoka nchi nyingi duniani
kwa kukaa kambi kwa pamoja, na hii itawasaidia vijana wetu kujifunza tamaduni za
nchi nyingi duniani”. Alisema Profesa
Na mwisho
profesa alipenda kuwashukuru IYF kwa kuleta wawezeshaji chuoni hapo kwani
huduma hii itawasaidia walio wengi chuoni hapo wakiwemo walimu wa shule za
msingi na sekondari kwa kupeleka elimu hii mashuleni kwao, na kwa wale ambao siyo walimu itawasaidia katika maeneo yao ya kazi.
No comments:
Post a Comment