Tuesday, February 27, 2018

ANGALIA HAPA KUJUA KILICHOTOKEA KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE NA UONGOZI

Wanawake kote nchini wametakiwa kuacha tofauti zao, wakae pamoja na kuangalia changamoto zinazowakabili na watafute namna ya kuzitatua ili waweze kusonga mbele.
Mbunge wa Hanang Mkoani Manyara Dkt. Marry Nagu akiongea na wanawake kutoka mikoa mbalimbali walioudhuria kongamano la wanawake na uongozi lililoandaliwa na TGNP Mtandao Mapema leo jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa mapema leo jijini Dar es salaam na Mh. Merry Nagu alipokuwa akifugua kongamano la siku moja la wanawake na uongozi lililoandaliwa na Mtandao wa jinsia TGNP.

Kongamano hilo lililofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam liliudhuliwa na watu wengi mashuhuri na wenye mchango mkubwa kwa taifa kama Mama Anna Makinda, Marry Rusimbi, Ester Bulaya Prof. Ruth Meena nk.

Katika kongamano hilo Marry Nagu alipenda kuwashauri kwa wale wanawake waliopata nafasi nzuri waweze kuzitumia nafasi hizo katika kuwanufaisha wanawake wenzao kama alivyofanya yeye.

“Wanawake wenye nafasi nzuri katika uongozi mnatakiwa kuzitumia nafasi hizo kuwakomboa wanawake wenzenu kama nilivyofanya mimi nilipokuwa Waziri wa Utumishi kwa kuweza kubadilisha sharia ya utumishi kutoka sharia ya serikali mchakato kwenda serikali matokeo” alisema Marry Nagu

“Katika ushiriki wa wanawake kwenye uongozi bado kuna changamoto katika kuchaguliwa au kupigiwa kura lakini wanawake tunatakiwa kuonyesha kwamba tunaweza na tuweze kutiana moyo wenyewe kwa wenyewe, kwani hii itawapa msukumo hata wanaume kuweza kutupigia kura kwa kuona umoja wetu” alisema Marry Nagu

Aidha Marry Nagu alipenda kuwashauri wanawake kuwa haitoshi kwa kusema wao ni wachakalikaji au wabangaizaji kwani mwisho wa siku wanakuwa hawana chochote wanachokipata na hivyo wanatakiwa kuwa wajasiliamari ili kujiongezea kipato katika maisha yao ya kila siku.

Na mwisho kabisa alipenda kumpongeza Rais Magufuri kwa kuona mchango na umuhimu wa wanawake katika serikali yake hata kumchagua Mama Samia Suluhu Hassan kuwa makamu wake, hii inaonyesha kwa kiasi gani rais anasogeza mbele harakati za wanawake.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema leo katika Kongamano la Wanawake na Uongozi lililoandaliwa na Mtandao huo Mlimani City jijini  Dar es salaam.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kujumuika, kushauriana/ kuelimishana kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake kote nchini.

Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa bado wanawake hawapewi nafasi ipasavyo kwani takwimu zinaonyesha kuwa hadi kufika oktoba 11 2017 wanawake waliyoweza kushika madaraka kama wakuu wa nchi ni 11 kati ya 178 na kwa afrika ni mwanamke mmoja tu ndio kiongozi wa juu yaani Rais.

Lakini pia Rwanda imekuwa ya kwanza kwa afrika mashariki na kidunia kwa asilimia 61.3 na Tanzania imekuwa ya pili kwa Afrika Mashariki lakini ya 25 kidunia kwa kuwa na asilimia 36.9 hivyo hali bado siyo nzuri katika usawa wa kijinsia.

Aidha Mkurugenzi huyo aliendelea kusisitiza swala la wanawake kuwezeshwa kiuchumi hii ikiwa ni pamoja na kazi za huduma ambazo zimekuwa ni kama majukumumu ya kawaida kwao bila kupata kipato chochote, wakati muda huo wangeutumia kutafuta kipato wengeweza kujenga uchumi wa nchi.

Na mwisho Lilian alipenda kushauri kuwa wanawake wapewe nafasi katika uongozi na maamuzi ili waweze kuonyesha uwezo wao katika Nyanja hizo kwani ushiriki wao umekuwa ni mdogo sana ukilinganishwa na wanaume kama wakuu wa Wilaya, Wabunge, Mawaziri na Wakuu wa Mikoa.

Mwenyekiti wa bodi wa TGNP Mtandao Visencia Shule akimkalibisha Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Hanang mkoani Manyara  Mama Marry Nagu mapema leo katika kongamano la wanawake na uongozi lililofanyika Mlimani City jijini Dar es salaam.
Waziri mstaafu ambaye pia Mbunge wa jimbo la Hanang mkoani Manyara Marry Nagu akijaribu kuwatia moyo wanawake wanaotamani kuwa kama yeye au watu wengine wakubwa ndani na nje ya Tanzania katika kongamano la wanawake na uongozi mapema leo jijini Dar es salaam .

Wageni mbalimbali waliofika katika Kongamano la Wanawake na uongozi lililoandaliwa na TGNP Mtandao mapema leo jijini Dar es salaam




                            ANGALIA HAPA KUJUA MENGI ZAIDI..
                   

No comments: