Sunday, February 4, 2018

WABUNGE WA VYAMA VYA UPINZANI WAENDA KUMUANGALIA SUNGU MAHABUSU

Wabunge wamefika Gereza Kuu la Ruanda jijini Mbeya kumjulia hali mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu'.
Tokeo la picha la mr, 2 sugu
Waliomtembelea Sugu ni mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema na wa Tandahimba (CUF), Katani Katani.

Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wapo mahabusu wakikabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Lema na Katani wakiongozwa na mwenyeji wao Mbunge wa  Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda pia wamefika nyumbani kwa Desderia Mbilinyi, mama mzazi wa Sugu eneo la Sae jijini Mbeya kwa ajili ya kumfariji na kumtia moyo kutokana na misukosuko anayopitia mtoto wake.

Wakizungumza na familia ya Sugu, wabunge hao wamesema yupo gerezani kwa kuwa anapigania haki za wananchi.

Lema amemtaka mama huyo kuwa na moyo wa uvumilivu.

No comments: