Sunday, February 25, 2018

WANAFUNZI MWENYEHERI ANUARITE WAPEWA MBINU ZA KUJIAJIRI

Wanafunzi  wa Shule ya Sekondari ya Mwenyeheri Anuarite iliyopo Kimara jijini Dar es Salaam, wamezipongeza mbinu mbalimbali za ziada wanazofundishwa na walimu wao  kwa ajili ya kujikwamua watakapomaliza masomo ili kujijengea maisha ya baadaye.


Wameyasema hayo katika hafla yao fupi iliyofanyika shuleni hapo iliyohusu namna wanavyoweza kutumia elimu zao watakapokuwa wamehitimu masomo  kabla ya kuajiriwa.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa shule hiyo, Carlos Mgumba,  alisema  lengo la shule yake ni kuwapatia elimu ya ziada ya kuelewa namna ambavyo wanafunzi wao wanaweza kujikwamua kiuchumi badala ya kusubiri kuajiriwa baada ya kumaliza elimu zao.

No comments: