Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kati) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwakabidhi baadhi ya washindi wa zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 walizoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 36 kutoka sehemu mbali mbali nchini walipata zawadi za simu janja kutoka Tigo katika promosheni hiyo inayoendelea ambapo wateja wa Tigo wanaonunua bando za intaneti kupitia menu *147*00* wanapata bonasi za bure hadi GB 1 za intaneti pamoja na fursa ya kushinda simu janja.
|
Wajinyakulia simu janja za TECNO R6 na bonasi za data bure- Zaidi ya simu 1,000 bado zinashandaniwa!
- Wateja wa kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania, wanazidi kufaidi zawadi za simu aina ya Tecno R6 pamoja na bonasi za data bure katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.
Akitangaza washindi 36 waliopatikana katika promosheni hiyo inayoendelea kwa kipindi cha miezi mitatu, Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa bado kuna simu zaidi ya 1,000 zinazoshindaniwa na wateja wa Tigo wanaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#.
‘Kufikia sasa tumepata jumla ya washindi 72 kutoka sehumu mbali mbali za nchi ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Lindi, Mtwara, Zanzibar, Arusha,, Pwani, Dodoma, Mwanza, Singida, Iringa, Mbeya na Tabora. Kwa hiyo nawahamasisha wateja wetu wote nchi nzima wazidi kununua bando za intaneti kuanzia shilingi 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# wapate nafasi ya kushinda mojawapo ya simu hizi bora zenye uwezo wa 4G,’ alisema.
Alibainisha kuwa ofa kabambe ya Nyaka Nyaka ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na mahitaji ya wateja na utakaowezesha kila mtu kufurahia huduma bora za mtandao wa Tigo 4G wenye kasi zaidi na ulioenea zaidi nchini.
Mmoja wa washindi, Ibrahim Mohammed Mtuliya, mkaazi wa Kigamboni Dar es Salaam alisema kuwa simu hiyo itamwezesha kupanua wigo wa biashara yake ya useremala kwa kupiga picha ya bidhaa zake nakuwatumia wateja kupitia mitandao ya jamii kama vile Facebook, WhatsApp na Instagram.
Katika promosheni hiyo murwa ya Nyaka Nyaka Bonus, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# wanapokea bonasi ya hadi 1GB intaneti bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Pamoja na haya, wateja hao pia wanapata nafasi ya kushinda mojawapo ya simu janja zaidi ya elfu moja zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 ambazo zinatolewa bure na Tigo kila saa.
Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.
No comments:
Post a Comment