Tuesday, March 13, 2018

MAPENZI YAMPONZA "MTEKWAJI" ABDUL NONDO,POLISI WASEMA ALIJITEKA

Tokeo la picha la mambo sasa
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetolea ufafanuzi kuhusu kile kinachoitwa kutekwa kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Nchini TSNP, Abdul Nondo.

Akizungumza na Wandishi wa Habari Kamanda wa Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa amesema mnamo Machi 7, mwaka huu waliletewa taarifa kutoka kwa wenzao wa Iringa ambapo walithibitisha kupatikana kwa mwanafunzi huyo akiwa mzima huku akiwa hajaripoti kituo chochote cha Polisi.

Mambosasa amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalumu kwa kushirikiana na wenzao wa Iringa walithibitisha kuwa Nondo hakutekwa bali alijiteka ambapo mawasiliano ya jumbe za simu yake zinaonesha kuwa alikuwa akiwasiliana na mpenzi wake aliyepo mkoani humo.

" Kijana huyu ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hakutekwa wala kushikiliwa bali alijiteka mwenyewe kwa nia ama ya kutafuta umarufu au kwa sababu ambazo anazijua mwenyewe,

" Jeshi la Polisi tunaendelea kutoa onyo kwa sababu hatutomuhurumia mtu yeyote ambaye anatafuta umaarufu kwa kuzua taharuki na wala hatutowapa nafasi ya kuharibu amani ya Nchi," amesema Kamanda Mambosasa.

No comments: