Jeshi la polisi mkoani Mwanza limewaonya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaotumia vibaya mitandao hiyo kufanya uharifu ikiwemo kuhamasisha maandamano yasiyo halali.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Naibu Kamishina Ahmed Msangi ametoa onyo hilo hii leo wakati akizungumza na askari waliokuwa kwenye mazoezi mbalimbali yaliyofanyika katika uwanja wa polisi Mabatini Jijini Mwanza.
Baadhi ya askari walioshiriki mazoezi hayo wameeleza kwamba yanawasaidia kuwa imara wakati wote na hivyo kutimiza vyema majukumu yao.
Kauli hii inakuja baada ya taarifa mbalimbali kuzagaa mitandaoni zikihamasisha wananchi kufanya maandamano ya amani Aprili 26 mwaka huu, siku ambayo ni Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo tayari maandamano hayo yamepigwa marufuku na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
BMG Habari-Pamoja Daima!
No comments:
Post a Comment