Mila ,desturi na elimu Katika Mtaa wa Basihaya Jijini Dar es salaam zimekuwa changamoto katika Mtaa huo kwani hata katika baadhi ya utatuzi wa matizo mbali mbali ya unyanyaswaji wa wanawake.
Marinus Albert ndule Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Basihaya ameyasema hayo wakati akiongea na habari 24 jijini Dar es salaam na kusisitiza kuwa ni vyema elimu ya jensia ikatolewa kuanzia ngazi ya Shule ya msingi kwani itasaidia watoto katika ukuaji wao kujua haki zao
Marinus Albert ndule Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Basihaya |
Pia amesema ni vyema elimu hiyo wakapewa watu wa jinsia zote wanaume na wanawake kwani kumpa mwanamke peke yake hakutasaidia kuondoa tatizo hilo
Ameongeza kwa kuwaomba wanawake kuripoti katika vituo vya sheria pindi wafanyiwapo uonevu kisheria na kusisitiza kwa kuomba msaada kwa serikali kumsaidia Bi Veronika Lukasi ambae ni mama wa pacha Watatu
Veronika ambae ni mjane na alifiwa na mume we akiwa na ujauzito wa mwezi mmoja na hatimaye alijifungua mapacha Watatu lakin hana msaada kutoka upande wowote na familia yake hawana uwezo kadhalika familia ya marehemu mumewe hawana uwezo
Bi Veronika ameomba msaada kwa serikali kwan hana makazi ya kuishi na watoto wake hao na wakati huo amepata tatizo la ugonjwa wa moyo.
No comments:
Post a Comment