Paparazi tayari
wameshaanzisha uvumi kama ilivyo ada, ambapo safari hii wakiihusisha kampuni
kinara katika uzalishaji wa simu za mkononi TECNO,ikitajwa zaidi midomoni mwa
watu, tetesi zaidi zinaihusisha kampuni hiyo pendwa na ujio wa toleo jipya
ikiwa ni muendelezo wa jamii ya Camon inayosemekana kuzinduliwa nchini Nigeria,
siku na saa bado havikuwekwa wazi.
Inasemekana
kwamba simu hiyo itaendana na uchumi wa Afrika ikikadiriwa kuwa na bei nafuu,
hivyo nadhani wa Afrika wanacho cha kujivunia.
Swali ni
kwamba je ni kweli TECNO watakuja na toleo jipya kama inavyosemekana midomoni
mwa wadau mbali mbali, bado hakujakuwa na taarifa rasmi kutoka kwenye vyanzo
vya kuaminika
Mara nyingi
TECNO inapohusishwa kuhusu toleo jipya bhaasi huwa kweli,je awamu hii TECNO
wanakipi cha tofauti? Maswali yamekua mengi yakiacha wadau vinywa wazi wakiwa
na shauku ya kutaka kuona ni nini TECNO watakachoingiza sokoni ikiwa ni
muendelezo wa Camon.
Kwa maelezo
zaidi tembelea tovuti ya http//www.tecno-mobile.com/tz
No comments:
Post a Comment