Friday, March 30, 2018

MBINU MPYA ZILIZOBUNIWA NA TGNP MTANDAO ZA KUFIKISHA UJUMBE KWA SERIKALI NA WANANCHI WAKE

Wanaharakati kutoka kata mbalimbali za jiji la Dar es salaam wakiwa katika makundi kuweza kujadili changamoto mbalimbali zilizopo nchini na namna ya kuzitafutia ufumbuzi kupitia bajeti ya mwaka 2018/19.

Baadhi ya wanaharakati wakiwa katika kundi wakijadili jambo fulani.

Wanaharakati kutoka kata mbalimbali wakijadiliana kuhusu bajeti ya mwaka 2018/2019 itakavyoweza kutatua changamoto zao.

Meza kuu ikipokea maswali kutoka kwa wananchi mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo lililofanyika mapema jana Makao Makuu ya Mtandao wa Jinsia (TGNP).

Mwananchi kutoka kata ya mabibo Anna Sangai akiomba ufafanuzi juu ya swala la kukatika kwa umeme pindi mvua zinaponyesha katika kata nyingi za jiji la Dar es salaam.
Mh. Altho Mwangoa akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya wananchi waliohuduria semina hiyo mapema jana makao makuu ya TGNP Mtandao jijini Dar es salaam.

Mh. Jackson Malangalila akijibu moja ya swali alililoulizwa na wananchi akiwa kama muwakilishi wa serikali na kutoa ufafanuzi juu ya mambo kadhaa ambayo wananchi wanaona hayapo sawa na kuamua kuwahoji viongozi wao.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa duku duku lake katika mkutano huo, akiwa ameshiriki kama mwananchi akiiwakilisha kata yake anayotoka.

Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP kufuatia mfurulizo wa semina zake za kila jumaa tano (GDSS) wamebuni mbinu mpya itakayowawezesha kufikisha ujumbe kwa urahisi kwa serikali na wananchi wake.

Mbinu hiyo iliyobuniwa na shirika hilo ni ya kusimamisha baadhi ya wafanyakazi wake kuwa kama viongozi wa serikali huku wakijibu maswali na kutoa ufafanuzi kwa wananchi kuhusiana na changamoto mbalimbali za kimaendeleo zinazoikabili nchi kwa sasa.

Katika semina hiyo iliyofanyika mapema wiki hii siku ya jumaa tano ya tarehe 29/03/2018 iliyoongozwa na mada isemayo mpango wa taifa wa maendeleo ya budget 2018/2019, Tanzania mpya ya ndoto yangu nitatoka?

Miongoni mwa maswali muhimu yaliyoulizwa na wananchi hao ni kuhusu swala la serikali kuongeza zahanati katika kila wilaya ikiwa zilizopo toka zamani zinalalamikiwa kuwa hazitoi huduma nzuri na vifaa tiba hakuna ikiwemo madawa ya kutosha.

lakini pia swala la utalii lilipata nafasi kubwa kwa wananchi kuhoji kuwa kwanini mpaka leo miundo mbinu haiboreshwi ikiwa barabara za kuelekea mbugani na sehemu nyingine zenye vivutio vya utalii.

katika sekta hiyo hiyo ya utalii ililalamikiwa kuwa inashindwa kujitangaza vizuri hii ikiwa ni hata kusababisha kuonekana kuwa mlima Kilimanjaro upo nchini Kenya na kusababisha nchi hiyo kupokea watalii wengi zaidi kuliko Tanzania ambao ndio wenye mlima wao.

Aidha katika maswali hayo swala la umeme liliendelea kuchukua nafasi kubwa kwa kuhoji kuwa kila siku serikali inaongezea nguvu katika swala hilo lakini bado changamoto za kukatika kwa umeme ziko pale pale hasa katika msimu huu wa mvua je tunavyosema uchumi wa viwanda tutaweza kufanikiwa ikiwa umeme wetu bado wa mashaka mashaka?

Na mwisho kabisa lilikuwa ni swala la hedhi salama kwa mtoto wa kike ambaye anakosa masomo kwa siku 4 mpaka 5 kwa kukosa taulo za na vyumba vya kujihifadhia, wananchi walitaka kujua serikali inalitazamaje swala hili.


No comments: