Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha Tigo, Hussein Sayed (kushoto) akipeana mkono wa pongezi na Mkuu wa Idara ya TTCL Pesa, Moses Alphonce mara baada ya makubaliano ya matumizi ya huduma za miamala ya makampuni hayo itakayowezesha mtumiaji kuingiza pesa moja kwa moja kwenye akaunti ya mtumiaji kwa gharama nafuu, hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam leo.
Shirika kubwa zaidi la kitanzania la mawasiano ya simu, na watoa
huduma ya simu zisizohamishika, broadband, bidhaa na huduma za internet
wanaoongoza Tanzania pamoja kampuni ya maisha ya kidigitali inayoongoza
Tanzania, Tigo. Leo wameingia katika ubia mkubwa, ambapo wateja kutoka katika
taasisi hizi mbili wataweza kutuma na kupokea fedha kati ya mitandao hiyo
miwili moja kwa moja katika akaunti zao.
Akiongea wakati wa kutangaza ubia huo katika ukumbi wa Golden
Jubilee Towers Jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Huduma za Fedha kwa njia
ya simu za mkononi wa TTCL, Moses Alphonce amesema kwamba, “Tunafuraha
sana kutia sahihi makubaliano ya ushirikiano huu ambao unaenda kuwanufaisha
wateja wetu na wananchi wote kwa ujumla. Ujio wa TTCL PESA katika sekta hii ya
mawasiliano ina lengo la kutengeneza ushirikishwaji wa masuluhisho ya kifedha
kwa watanzania wote. Lengo letu ni kubadilisha mahitaji ya kila siku ya kifedha
ya watu wetu yawe yasiyo ya fedha tasilimu na kuwa wawezeshaji wa miamala yote
ya kidigitali inayofanyika Tanzania”.
Aliongezea kuwa, tuna mifumo bora sana ambayo inaweza kutoa uwezo
kwa makampuni na taasisi za kiserikali uwezo wa kutoa malipo ya kidigitali kwa
mamilioni ya watanzania.
TTCL PESA inatoa huduma ya kifedha ya kidigitali ambayo ni bei
nafuu, ya haraka na salama ambayo inazidi huduma za benki kupitia simu za
mkononi, huduma za malipo, kuongeza muda wa maongezi na uhamishaji wa fedha.
Kwa upande wake, Afisa mkuu wa Huduma za kifedha za simu za
mkononi wa Tigo, Hussein Sayed amesema kwamba makubaliano haya kuwa ni
mwanzo wa ushirikiano mkubwa lakini pia jukumu la uanzilishi la Tigo katika
huduma za fedha kupitia simu za mkononi, ushirikiano tayari umeshasainiwa.
Jambo hili limeziakikishia kampuni hizi mbili zenye shauku ya kuwapatia wateja
wao huduma ya kiwango cha juu katika zama hizi za huduma za kifedha za
kidigitali. “Kwa makubaliano haya kwa mara nyingine tena tunaisaidia Tanzania
kuimarisha jukumu lake lisiliokwepeka katika waanzailishi wa ushirikishwaji wa
kifedha kwa njia za kidigitali duniani. Ushirikiano mara zote huwa ni chachu ya
ukuaji katika sekta ya fedha kwa njia za simu za mkononi.” Alisema Sayed.
“Tumetambulisha sokoni idadi kadhaa ya bidhaa zenye ubunifu na
tuna nia ya kupanua watumiaji wetu kwa kushirikiana na watoa huduma wenzetu
walioko sokoni” Aliongeza Hussein.
Katika mwezi June 2014, Tigo iliibuka kuwa ya kwanza baada ya
kufanikiwa kuzindua makubaliano ya ushirikiano ya kwanza ya aina yake ambayo
yanawawezesha mamilioni ya wateja wa Tigo Pesa kutuma fedha na kupokea fedha
kwa watoa huduma wengine waliosajiliwa.
No comments:
Post a Comment