Wachezaji
wa mpira wa miguu chipukizi wa Afrika waliochaguliwa kutoka nchi za Ghana,
Ivory Coast na Cameroun tarehe 31 August 2019, wameeleza fursa hiyo ya pekee na
yenye kuhamasisha wakati wa mahojiano na vyombo vya habari jijini Abidjan, mji
mkuu wa Ivory Coast. QNET iliwaalika waandishi wa habari katika mechi ya kupeana
uzoefu kati ya Manchester City FC na Brighton & Hove Albion; Waandishi hao
walitazama ligi ya mabingwa na kuzungumza na wachezaji chipukizi kutoka
Afrika.
QNET
kampuni ya biashara ya mtandao inayoongoza ulimwenguni, kama sehemu ya jitihada
zake za kuendeleza vipaji na kama namna ya kurudisha fadhila kwa jamii ambako inafanyia
kazi, imedhamini wachezaji watatu vijana wa kiafrika kwenda kuhudhuria programu
ya Lugha na Mpira wa Miguu ya kipindi cha msimu wa joto katika shule ya mpira
wa miguu cha Manchester City jijini Manchester. Programu hii ilikua ya wiki
mbili yenye lengo la kuhamasisha na kufundisha mpira wa miguu na kozi ya Lugha
ya Kiingereza kwa wachezaji chipukizi wenye umri kati ya miaka 12-17. Programu
hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 28 Julai mpaka tarehe 12 Agosti, 2019 katikati
ya viwanja vya mafunzo vya timu ya Manchester City katika shule ya Mpira wa
Miguu ya klabu ya City.
Kwa
mujibu wa Hamza Gaveh, wachezaji chipukizi kutoka Ghana walisema: "Ilikuwa
ni moja kati ya wakati mzuri sana katika maisha yangu. Nimepata fursa ya kupata mafunzo pamoja na
klabu bora zaidi ya mpira wa miguu katika mashindano ya ligi za uingereza. Nimejifunza mengi kutoka katika vipindi vya
mpira na kutoka katika vipindi vya Lugha ya Kiingereza. Nilikuwa kinara katika
darasa langu la lugha ya kiingereza na katika michezo, nimejifunza zaidi kuhusu
kufanya kazi kwa pamoja katika timu na mikakati ya kijihami. Nimepata marafiki wapya kutoka sehemu
mbalimbali duniani ikiwemo Urusi na katika nchi za Sacandinavia."
Baba
Ndiaye kutoka Ivory Cost amesema: "Japo kuwa nimesafiri sehemu kadhaa kucheza
mpira wa miguu, Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester City ni sehemu bora zaidi
kati ya zote nilizowahi kwenda. Baada ya vipindi vya kuhamasisha tulivyovipata,
sasa ninajihisi kwa kiasi kikubwa kwamba siku moja nataka kuchezea klabu ya
manchester City. Ninafanya vizuri sana darasani na natumaini kufanya vizuri
katika mpira wa miguu na kuchezea Ligi ya Maibingwa uingereza.
Na Yvan
Noh Nafeng kutoka Cameroun kwa furaha kubwa alisimulia: "Sikuwahi kusafiri kwa ndege hapo awali
na ilikuwa ni mara ya kwanza kupata hati ya kusafiria ya kimataifa. Tukio zima
hili lilikuwa ni kitu kikubwa sana ambacho hakijawahi kutokea maishani mwangu. Nawafahamu
wachezaji wengi chipukizi kutoka katika klabu yangu ya mpira wa miguu nchini
Cameroun wanaotaka kuwa kama mimi, nimepanga kubakia na tabia njema na kuwa
makini. Vile vile ninapanga kuwafundisha
wenzangu baadhi ya masomo ya mpira wa miguu niliyojifunza".
Akiongea
katika sherehe, Bwana Rajesh Rao, Mkurugenzi wa Mkuu wa QNET wa Mahusiano ya
Kimataifa, alisema. "Programu hii ni sehemu ya jitihada za QNET za
kuendeleza vipaji, kurudisha kwa jamii ambako tunaendesha shughuli zetu pamoja
na jamii kwa ujumla. Tunaamini kwamba
fursa waliyopata kutoka Klabu ya Manchester City FC imewahamasisha vijana hawa kutafuta
viwango vya juu katika maisha yao".
Akiongea
kuhusu ushirikiano kati ya Manchester City, QNET na programu ya mpira wa miguu,
Bwana Biram Fall, Meneja Mkuu wa QNET kanda ya Afrika, amesema "QNET ni
biashara ambayo inaamini na kudumisha uendelevu. Tunaamini katika kuendeleza na
kukuza vipaji katika ngazi zote.
Udhamini wa Klabu ya mpira wa miguu ya Manchester City kama mshirika wa
mauzo ya moja kwa moja na mdhamini wa lebo za mikononi (Sleeve Sponsor) ni moja kati ya jitihada zetu katika mpira wa miguu
pamoja na hamasa ambayo mpira huo unaambatana nao duniani kote. Kupitia
Ushirikiano huu, tumepata fursa ya kupeleka watoto wanaotokea katika familia
zenye kipato cha chini Afrika kwenda katika klabu za mpira wa miguu na shule ya
lugha ya kiingereza jijini Manchester; jambo hili kweli limebadilisha maisha ya
watoto hawa, Watoto tunaowasherehekea
leo ni matunda ya ushirikiano huu.
Tunatumaini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja na kutafuta njia
mpya za kibunifu za kushirikiana na kuwafikia wadau wetu wote."
QNET inaendelea kupanua uwepo wake katika sehemu mbalimbali
katika bara la Afrika ikiwemo Tanzania ambako inatoa fursa za ujasiriamali kwa
watu na kuwasaidia kubadilisha maisha yao kuwa bora zaidi. Mbali na ushirika
katika michezo, QNET vile vile ni kampuni ambayo imewekeza katika kuwajibika
kwa jamii, kurudisha na kutoa kwaajili ya manufaa ya jamii na jambo hili
linafanyika katika maeneo yote ambako QNET inaendesha shughuli zake. Katika
mwezi Novemba mwaka 2018, Kampuni ya
QNET ilitunukiwa tuzo ya e-Commerce CSR Company kuwa ni kampuni bora ya
biashara ya mtando kwa mwaka huo, ambayo ilitolewa na Kituo cha Uwajibikaji wa
Mashirka kwa Jamii cha Afrika Magharibi (Centre for Corporate Social
Responsibility West Africa.)
No comments:
Post a Comment