Wateja 84 wajinyakulia simu janja za TECNO R6 na bonasi za
data bure baada ya kununua bando za intaneti kupitia *147*00#
Zaidi ya simu 840 pamoja na bonasi za uhakika za intaneti
bado zinashindaniwa!
Dar es Salaam, Machi 9, 2018 – Kampuni inayoongoza kwa
mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania, leo imewazawadia washindi 84 wapya wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus simu aina
ya Tecno R6 zenye uwezo wa 4G.
Akikabidhi zawadi hizo kwa baadhi ya washindi katika hafla
fupi iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo, Mtaalam wa
usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza alisema kuwa kufikia sasa promosheni
hiyo imeibua washindi wa simu 240 kutoka sehemu mbalimbali za nchi.
‘Kila anayenunua bando la intaneti kuanzia TZS 1,000 kupita *147*00# anapokea bonasi ya
hadi 1GB intaneti bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp,
Instagram ama Twitter. Pia anaingizwa kwenye droo ya kushinda mojawapo ya simu
zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 zinazoshindaniwa katika promosheni hii ya
Nyaka Nyaka Bonus.’
‘Nina furaha kubwa kupokea simu hii kutoka Tigo,
itakayoniwezesha kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki kwa kasi ya juu ya
4G,’ Jasper Dethuel Kimei, mfanyabiashara na mkaazi wa Vingunguti Dar es Salaam
alisema baada ya kupokea zawadi yake ya simu.
“Tunawakaribisha
wateja wote wa Tigo kuchangamkia fursa hii kwani baio tuna simu 840
zinazozubiri kunyakuliwa katika promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus,’ alisema
balozi wa promosheni hiyo, Meena Ali.
Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza
idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.
No comments:
Post a Comment