Wanawake kote
nchini wametakiwa kuwa na umoja na kujenga utamaduni wa kusaidiana bila
kuangalia itikadi zao za vyama au dini, kwani wanawake wote duniani wana sifa
zinazoshabihiana na matatizo yanayofanana.
Spika wa Bunge Mstafu Anna Makinda akiongea na Madiwani pamoja wanaharakati kutoka kata mbalimbali za jiji la Dar es salaam. |
Hayo yamesemwa mapema leo jijini Dar es salaam na Spika wa bunge mstaafu Mh. Anna Makinda alipokuwa akifungua warsha maalumu ya madiwani wanawake wa jiji la dar es salaam iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP).
Mh. Makinda
alisema kuwa madiwani wanawake mnatakiwa kuwa na umoja ulio imara kama wa
wabunge wanawake ambao umoja huo una lengo la kusaidiana kuhakikisha wanawake
wanaendelea kufanya vizuri katika uongozi bila kujali itikadi za vyama vyao.
“Sababu za
kuundwa kwa umoja huu ilikuwa ni kuleta ukombozi kwa wanawake kwa kuangalia
changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja bila kuangalia
itikadi za vyama huku lengo likiwa ni kufikia malengo ya kuwa na usawa wa
kijinsia kati ya wanaume na wanawake”. Alisema Makinda
Aidha Mh.
Makinda alisema kuwa wanawake wanaweza kuongoza vizuri kuliko wanaume kwani
mwanamke akiwa Diwani au Mbunge katika eneo analolitumikia ataweka vipaumbele
kwenye huduma za jamii kama Maji, Afya, Elimu kwa kuwa anazijua vizuri
changamoto zinazowakabili wanawake wenzake kwa kuwa na yeye amepitia changamoto
kama hizo.
Semina ikiendelea kutolewa. |
Spika huyo mstaafu aliendelea kusema kuwa katika kugombea nafasi mbalimbali kunakuwa na changamoto nyingi zinazowapata wanawake lakini mnachotakiwa ni kutokubali kukatishwa tamaa, kwani mtasikia maneno mengi na wengine watasema mnaenda kutafuta mabwana na siyo uongozi kwani mara nyingi harakati kama hizi wengi wanazihusisha na mambo ya kihuni.
Na mwisho
aliwashauri madiwani hao kuwa wasikubali kuachia nafasi za kwa kushindwa na
wapinzania wao ila wanachotakiwa kukifanya ni kujipanga vizuri mpaka watakapo
amua kuachia wenyewe kama alivyo fanya yeye katika jimbo lake.
“Itakuwa nia
aibu sana wewe uliyekuwa ndani kutolewa na mtu aliye nje madiwani wanawake
mnatakiwa kusimama imara kutetea nafasi zenu msikubali kutetereshwa na wanaume
mpaka mtakapo amua kuachia wenyewe kama nilivyofanya mimi katika jimbo langu”
alisema Makinda
Kwa upande
wake Mkuu wa idara ya Ujenzi wa nguvu za pamoja wa TGNP Mtandao Bi. Grace
Kisetu alisema kuwa wao kama shirika la kutetea haki za wanawake wapo katika
mpango kabambe wa kupigania ongezeko la wanawake katika nafasi za uongozi na
maamuzi.
Aidha Dada
Grace alisema kuwa mwaka 2016 disemba serikali ilipitisha mpango mkakati wa
kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto na muongozo uliotolewa
unaonyesha watekelezaji ni taasisi binafsi kama TGNP na halmashauri imepewa
jukumu kubwa la kusimamia mpango huu.
Grace
aliendelea kusema kuwa wao kama TGNP wana jukumu la kufanya chambuzi za bajeti
mbalimbali za kisekta na hata bajeti kuu kwa kuangalia upande wa wanawake na
watoto wanaangaliwa vipi na bajeti hizo.
Aliongezea
kuwa miongoni agenda zetu itakuwa ni kujadili kwa fedha ambazo zilikuwa
zikitengwa kwa ajili ya wanawake na vijana ambapo hapo mwanzo mgawanyo ulikuwa
ni 5% kwa wanawake na 5% ilikuwa kwa vijana na haikutosha, lakini kwa sasa
imegawanywa upya na kuwa 4% kwa wanawake na 4% kwa vijana na 2% iliyobaki
kupelekwa kwenye kundi la watu wenye ulemavu.
No comments:
Post a Comment