zipo taarifa kuwa baadhi ya wananchi Mkoa wa Mjini
Magharibi wanatumia, wanashiriki, wanafadhili au kusaidia biashara ya madawa ya
kulevya kama ilivyo kwenye maeneo mengine nchini.
Hata hivyo Serikali ipo kwenye vita kali ya kupambana na mtandao wa madawa
ya kulevya na Inspekta Jenerali wa Polisi kwa kushirikiana na Kamisheni ya Polisi
Zanzibar waliunda timu kutoka Kitengo cha Operesheni Maalum za Polisi Makao
Makuu Dar es salaam kuja kuongeza nguvu katika ufuatiliaji wa kero hii kama ilivyo
kwenye maeneo mengine ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
katika oparation hiyo kumeweza kubaini taarifa na kuwakamata watu kadhaa wanaohusika kwa namna moja au nyingine kwa kutumia, kuuza, kufadhili au kusaidia na mpaka sasa jumla ya watuhumiwa 105 wamekamatwa.
Na katika hao watuhumiwa walioshikiliwa waliopatikana na hatia ni 58 ambao kati ya hao watuhumiwa 26 wamefikishwa mahakamani tayari, na watuhumiwa 16 bado wako chini ya upelelezi na 16 wengine wapo chini ya uangalizi wa polisi(police supervisee.
Na vielelezo vilivyopatikana ni Heroin kete 1293 na vifuko vitatu ambavyo ni sawa na gramu 74.385 na banghi vifurushi 373 na nyingine vifuko vitatu.
Wito kwa wananchi wote
Tahadhari kwa wananchi wote
wanaohusika kwenye mtandao huu kuacha mara moja kwa kuwa vita hii imeshaanza na
inaendelea kwa lengo la kuhakikisha usalama wa vizazi vilivyopo na vizazi
vijavyo maana madawa haya yanaathiri zaidi vijana ambao ndiyo muhimili na nguvu
kazi ya Taifa.
Aidha nawapongeza wananchi wote waliotoa ushirikiano wa kutoa
taarifa za uhalifu
huu bila ya kuona muhali. Niwaombe wananchi wote
kuendelea na ushirikiano huu
wa kutoa taarifa.
Mwisho natuma salamu kwa watuhumiwa
wote waliotoroka kule
walipo wajue kuwa wanatafutwa na watakamatwa ili wahojiwe
na
hatimae kufikishwa Mahakamani.
Liberatus Sabas – DCP
Mkuu Wa Uperesheni Maalum za Polisi Tanzania
21.03.2018
No comments:
Post a Comment