Friday, March 16, 2018

WIKI YA MAJI YAZINDULIWA MAPEMA LEO NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM POUL MAKONDA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Mh. Paul Makonda amelitaka Shirika la Maji Safi na Maji Taka  DAWASCO kuhakikisha linashughulikia  kero zote za maji  kwa Wananchi ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na kupatia ufumbuzi  tatizo la Maji Taka  yanayotiririka holela kwenye  makazi ya watu.
Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la maji safi na maji taka DAWASCO wakifuatilia uzinduzi wa Wiki ya Maji uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam na kuzinduliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Poul Makonda.

Makonda ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa  Wiki ya Maji  ambapo amesema tatizo la  maji taka  limekuwa   kero sugu  katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo  jambo linalohatarisha hata Afya za wananchi.

Aidha  Mhe,  Makonda  ameitaka  DAWASCO  kuongeza jitihada za kufikisha huduma ya maji kwa wananchi ili kuenda sambamba na  sera ya Serikali ya awamu ya Tano ya kumtua mama ndoo kichwani.

Hata hivyo  Makonda  ametoa wito kwa watumishi wa  DAWASCO wanaokwenda kusoma mita  kwa wananchi kuwa na lugha nzuri  kwa wananchi pamoja na kushughulikia  kero ya wananchi kubambikiziwa kiwango kikubwa cha malipo ya bili za maji.

Kuhusu changamoto ya  upotevu wa maji Mhe, Makonda  amelitaka shirika hilo kulipatia majibu ya haraka tatizo hilo ili kiasi cha maji yanayopotea kiweze kuwahudumia wananchi.

Ili kufikisha huduma ya maji kwa  maeneo yenye changamoto RC Makonda  amejitolea kuchimba  visima 50  vya maji ambapo amewasihi Wenyeviti wa mitaa hiyo kuainisha maeneo ya  kuchimba visima hivyo.

Pamoja na hayo Makonda  ametaka uwepo wa  ushirikiano wa kikazi baina ya TANROAD, TANESCO, TARURA na DAWASCO  ili kumaliza changamoto ya kukatwa kwa miundombinu ya maji  wakati wa ujenzi wa barabara pamoja na  uharibifu wa barabara.
Meya wa jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Mwita akitoa mchango wake kuhusiana na Uzinduzi wa Wiki ya maji, pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Poul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Poul Makonda akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema leo jijini Dar es salaam katika Uzinduzi wa Wiki ya Maji.
Baadhi ya wadau walioudhuria mkutano huo.

No comments: