Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Huduma kwa Wateja Mercedes Benz Trucks Africa, Torsten Bauerheim (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar Es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa Malori mapya ya kisasa ya Mercedes Benz aina ya Actros na Arocs. Wengine kwenye picha kutoka kushoto ni Meneja Chapa wa Mercedes Benz Tanzania, Jerome Sentimea, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CFAO Motors, Marius Prinsloo na Maneja Mauzo wa MB Trucks Africa, Hansjorg Richter |
· Mercedes-Benz
inapeleka mbele historia ya malori yenye nguvu nchini TANZANIA
· Malori yote mapya aina ya
Actros na Arocs yamezinguliwa
Tarehe
8/02/2019 Jijini Dar es salaam. Actros
mpya kabisa: Ni malori ya kuaminika na yenye ufanisi kwaajili ya masafa marefu
na usamabazaji yamezinduliwa leo katika mji mkuu wa Tanzania.
Akiongea katika
hafla hiyo ya kupendeza, Mkurugenzi wa Mauzo na Huduma kwa Wateja wa Malori ya
Mercedes Benz Afrika Bwana Mr Torsten
Bauerheim akisema, 'Malori yote mapya ya Actros na Acros yanakuja na injini
yenye ufanisi yenye silinda 6 katika mstari, vyumba vya dereva vya kisaa
vinavyoruhusu hewa kupita na Mercedes PowerShift 3 ya kisasa, injini ya
kujiendesha yenyewe zikiwa na miundo mbalimbali tofauti kutegemeana na
mazingira ya kanda husika. Aliongeza
kuwa, Malori yote mapya ya Actros ni ya kuaminika na ya uhakika kwaajili ya
ujenzi na matumizi katika barabara za vumbi na zote zimepitia majaribio makali
ya ubora ya zaidi ya kilomitea milioni 60 kabla ya kufanya uzinduzi wa soko.
Mkurugenzi Mtendaji wa
wasambazaji walioithibishwa wa Mercedes-Benz, CFAO Motors Tanzania Ltd, Bwana Marius Prinsloo amesema kwamba 'Maloti
mapya ya Actros na Arocs yanatoa kiwango cha ziada cha uimara, ufanisi katika
matoleo ya malori ya Mercedes-Benz Yakiwa yametengenezwa katika kiwanda cha
malori kikubwa kuliko vyote duniani nchini Ujerumani, Malori haya yanakuja
katika aina mbalimbali mahususi kwaajili ya soko letu la Tanzania - yakiwa
yamebuniwa na kutengenezwa kuhimili mazingira magumu ya uendeshaji.
Yamejaribiwa kwa kina duniani
kote, katika barabara za aina zote na katika mazingira magumu zaidi, magari
haya ni mifumo bora zaidi kwaajili ya kazi ngumu. Majaribio yalijumuisha jumla
ya zaidi ya kilometa milioni 6 za mbio za ustahimilivu zilizofanywa na kituo
cha majaribio ya malori ya Mercedes-Benznchini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za
Kiarabu.
Aliongeza kuwa 'Chumba kipya cha
pekee cha dereva kinajivunia kiwango cha juu cha vifaa na mazingira mazuri ya
ndani, wakati uendeshaji ni rahisi na wakustarehesha . Aina zote mbili za
malori ya Actros na Arocs zinavutia kwa teknolojia ya kisasa zaidi na mfumo wa
kuaminika wa uendeshaji kutokea chanzo kimoja.
Injini zenye ustahimilivu, zenye nguvu na zenye ufanisi zinapatikana
katika aina za utoaji moshi wa Euro III, IV na V, ikiwa inatoa aina mbalimbali
za nguvu ya msukumo kuanzia 240 kW (326 hp) mpaka 460 kW (625 hp). Ikiwa
imeunganishwa na toleo la hivi karibuni la Mercedes PowerShift 3, gia boksi ya
kujiendesha yenyewe, malori ya Actros na Arocs yanafikia kiwango cha juu cha
ufanisi wa mafuta, ikiwa inachangia kuongeza faida za uendeshaji
Actros mpya zimetengenezwa
kwaajili ya usafirishaji wa masafa marefu pamoja na usambazaji wa mizigo
mizito. Zinapatikana na mpaka aina 22 tofauti za chumba cha dereva na zinakuja
katika matoleo ya chuma au ya kushikiliwa na upepo. Kwaajili ya mazingira
magumu ya uendeshaji, Actros zinapatikana katika injini zenye nguvu za 15.61 na
kasi ya 16 na gia boksi ya kujiendesha yenyewe ya Mercedes PowerShift 3
'Arocs mpya ya kustaajabisha iko
kwaajili yako pale utakapo kuwa unahitaji ustadi wa kipekee - iwe katika
shughuli za ujenzi mbali na barabara za lami. Malori ya Arocs yenye
ustahimilivu mkubwa yanaweza kufanya kazi katika mazingira magumu zaidi ya barabara
za vumbi mbali na bara bara za lami. Arocs zinapatikana kama Chassis-, Mixer-,
Tipper- na aina mbalimbali za uendeshaji - kuanzia miundo ya 4x2 mpaka 8x8 na
uzito (GCW) wa mpaka kufika tani 250.
Kwa kudokeza, Actros na Arocs
yanaweka viwango vipya pale inapokuja kuhusu suala la usalama na mifumo ya
usaidizi, inayomsaidia dereva na kuokoa maisha. Bwana Torsten Bauerheim alihitimisha.
No comments:
Post a Comment