Henrik Krag kutoka Zonith akiwa na askari wa kampuni ya Q4S akielezea jambo kwa wageni waalikwa |
Inj.Omar Bakar kutoka Tanzania Data Lab akiwasilisha mada
kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma mpya za Teknolojia ya ulinzi wa kisasa zenye
kulinda watu na mali zao kutoka kampuni ya G4S Tanzania.
|
Sugandran wa Geo Tab akiwasilisha mada kwa wageni waalikwa
|
·
G4S
inatoa huduma za ulinzi zinazotumia teknolojia kusaidia taasisi na watu binafsi
kulinda watu na mali zao.
Tarehe 8 Februari 2019, Dar es
salaam. Wakati ambapo ni muhimu kupunguza gharama za uendeshaji, sio tu kwamba
teknolojia itasaidia kufikia malengo haya lakini pia itaweza kutoa manufaa
zaidi ya kuaminika na ufanisi. Kwa
kuongezea zaidi matuko mengi ya matumizi ya teknolojia inayostahili imeweza
kuondoa maofisa wa ulinzi katika maeneo ambayo kuna hatari ya watu kuumia.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa
teknolojia mpya ya ulinzi inayotolewa na G4S, Balozi wa Denmark Mhe. Einar H.
Jensen alisema kwamba uimarishaji wa usalama wa watu na mali zao katika kanda
hili umekuja katika wakati muafaka kwaajili ya kukabiliana na vitisho
vilivyoshuhudiwa hivi karibuni. 'Dunia
inabadilika kwa kasi sana na mahitaji ya kulinda watu na rasilimali hayajawahi
kuwa makubwa kama hivi sasa. Mahitaji ya usalama kwa watu wa Afrika Mashariki
vile vile yanazidi kuongezeka. Si muda mrefu tulikabiliana na uvamizi wa
kikatili wa magaidi katika hoteli nchini Kenya, tunapaswa kuwa tayari kwa
mashambulizi ya aina hiyo katika siku zijazo.
Akitangaza uzinduzi wa bidhaa
za kisasa mwaka 2019, Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa G4S Secure Solutions
Tanzania, Andrew Lauwo amesema 'Mfumo wa Ulinzi wa ishara ya kengele ya video (A video
alarm security system) (Videofied) iliyotengenezwa Ufaransa yenye uwezo wa
kuhisi mtu anapoingia na kisha kutuma video ya haraka kwenye control room ya
G4S na kwenye simu yako pale mtu anapoingia katika sehemu husika ni bidhaa
nyingine iliyoko katika ofa: Mfumo huu unatumia betri na hauna waya na unaweza
kufungwa nje au ndani. Mfumo wa VIDEOFIED
unatumika zaidi kulinda mali na pia unatumika katika mazingira ya nje kama vile
sehemu za kuhifadhia boti, maeneo ya burudani ya nje, katika njia na sehemu
nyingine ambako nishati ya umeme hakuna.'
'At the Gate' (Katika Mageti)
ni mfumo wa kudhibiti waingiaji ambao unaruhusu ufuatiliaji wa nani anaingia na
kutoka katika eneo lako kwa kuskani magari na taarifa za leseni za madereva
wanapoingia na kutoka kupitia kifaa cha Android. Kifaa hiki kinafanyakazi kwa kutumia mtandao
wa simu au kuunganishwa na Wi-Fi na kutoa vipengele mbalimbali vinavyokutaarifu
mgeni anapofika getini, picha nyingi za magari na walioko ndani, taarifa za
laptop, silaha,simu za smart, tablets nk. zinazoingia na kutoka katika eneo
nk.'. aliongeza.
Akitolea maoni kuhusu mfumo wa
kufuatilia magari (Vehicle Tracking Management System) alisema, ‘Geotab kutoka Canada: ni mfumo wa
kufuatilia magari na kufuatilia tabia za dereva ambao pia unatoa kifaa cha
ufahamu wa dereva (Driver Awareness tool) kinachobadilisha jinsi mafunzo ya
mereva yanavyofanyika wakati wa kuendesha kwa kutoa maelekezo ya sauti ya hapo
kwa hapo kwa dereva. Zaidi ya eneo halisi gari liliko, taarifa za kasi ya gari
idadi ya tripu na umbali ambao tayari ameshasafiri, utendaji wa dereva kama
vile kufunga breki kwa haraka, kukata kona na takwimu za utulivu wa kupita
kiasi pia zinapatikana. Mfumo huu
umetengenezwa kusimamia na kufuatilia utendaji wa gari, tabia za dereva na
kuboresha mifumo ya usalama.'
Vilevile alisema kwamba, ‘The Sentinel Perimeter Protection
kutoka Afrika ya Kusini ni mfumo wa masafa marefu wa kutambua uvunjaji na
kuzuia ambao unatoa ishara ya kengele unapokuwa umekiukwa na kutuma video za
tukio kwa kutumia Wi-Fi wakati pia ikiwa inatuma ishara ya tahadhari kwenye
Control room yetu na katika simu yako ya mkononi masaa 24/7 Ina uwezo wa
kusimamia eneo la mita 150 na vipengele vya ziada vinaweza kuongezwa kwenye
mfumo huu kutoa ulinzi wa asilimia 100% katika eneo husika.
Akiongea kuhusu mfumo wa
ulinzi kwa kutimia video ulioko katika ofa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa ZONITH,
Kristian H Stiesmark amesema kwamba 'Ishara ya Kengele ya Hofu Binafsi (Personal Panic Alarms) iliyoundwa na
ZONITH, kampuni ya teknolijia ya kiwango cha juu ya watu wa Denmark inatoa
kifaa cha kutolea ishara ya kengele ya hofu binafsi cha kufunga mahali na cha
kutembea nacho ambacho kinamruhusu mtumiaji kuita msaada kutoka katika kikosi
cha kuitikia matukio cha G4S panapotokea vitisho vya kiusalama au huduma ya kimatibabu
au dharura ya moto. Zonith inatoa teknolojia ya kuchagua inayotumia Bluetooth
ambayo inaruhusu ishara ya kengele na sehemu ulipo kutumwa kutokea sehemu
yoyote ambako mtandao wa GSM
unapatikana.'
No comments:
Post a Comment