Monday, June 20, 2022

ACT Wazalendo yataka ukaguzi maalum, kufuatia hasara ya Bilion 208 TADB.

Tarehe 16 Juni 2022, ACT Wazalendo tulifanya uchambuzi wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23. Katika uchambuzi wetu miongoni mwa mambo tuliyoyabainisha ni kutaka uwajibikaji kutokana na hasara iliyopatikana kwenye Sakata la korosho mwaka 2018. 

Hoja yetu ilitokana na Taarifa ya Uchumi wa Taifa 2021 iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Nchemba, iliyosema kuwa Serikali imelibeba deni hili la TADB lenye thamani ya shilingi bilioni 208 ambazo zilikopwa kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB), kwa kuligeuza kuwa mtaji wa TADB (coversion). 

Jumamosi tarehe 18, Juni 2022 Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kupitia mitandao ya kijamii na tovuti yake, ilikanusha kuwa hakuna hasara yoyote iliyopata kutokana na sakata la korosho kwa kuwa fedha zilizokopwa zilikuwa na lengo la kukuza mtaji wa benki hiyo na siyo kununua korosho. 

ACT Wazalendo bado tunataka uwajibikaji katika suala hili na tunamshauri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) afanye ukaguzi maalum wa ushiriki wa TADB katika kununua Korosho mwaka 2018/19 na matumizi ya mkopo huu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). 

Imetolewa na: Ndugu Juma Kombo

jkombo@actwazalendo.or.tz 

Naibu wa Sekta ya Fedha na Uchumi - ACT Wazalendo 

20.06. 022.

No comments: